
Nchini Madagascar, hatua mpya imepigwa kuelekea ujenzi wa kituo kikubwa zaidi cha kuzalisha umeme nchini humo. Wiki hii, Serikali imetangaza rasmi uwekezaji wake katika muungano unaohusika na majaribio ya mradi huo, ulioko Sahofika, katikati mwa nchi, kwenye Mto Onive. Hatua kubwa ya mageuzi, baada ya zaidi ya miaka sita ya kuchelewa. Pamoja na 85% ya wakazi ambao hawana umeme, ujenzi wa mtambo huu wa kuzalisha umeme unaweza kukidhi kwa kiasi mahitaji makubwa ya nishati nchini.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Muundo wa umiliki wa mradi wa Sahofika hatimaye umeanzishwa. Kwa kununua 49% ya hisa kupitia kampuni ya Malagasy Sovereign Fund SA, serikali ya Madagascar wiki hii imekuwa mbia wa tatu kujiunga na muungano wa Neho, pamoja na Themis na Eranove, waendelezaji wawili wa Afrika waliobobea katika miradi ya nishati barani Afrika.
Kujiunga kwa Madagascar katika umiliki wa hisa kunapaswa kuwezesha muungano kupata mikopo kwa viwango vya upendeleo. Kwa maana hii sasa ndio kiini cha vita. Inakadiriwa kuwa euro bilioni moja, mradi unahusisha ujenzi wa bwawa la kuzalisha umeme, kiwanda cha uzalishaji, kilomita 60 za barabara ya kuingia, njia ya maji ya kilomita 4 na milingoti miwili mikubwa. Miundombinu mingi sana iyohitaji usaidizi mkubwa wa kifedha.
“Hatuanzii kutoka mwanzo, mbali nayo,” kinafichua chanzo kilicho karibu na kesi hiyo. Hakika, kabla ya janga la Covid-19, karibu wawekezaji kumi na tano walikuwa tayari wameonyesha nia yao. Leo, ni kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika – inayosimamia mpango wa kifedha – na muungano wa Neho kuwashawishi kjihumiza tena.
Jirama, mteja wa kimkakati na dhaifu
Jirama, kampuni ya umma ya maji na umeme ya Madagascar, itakuwa mnunuzi wa kipekee wa nishati inayozalishwa na Sahofika. Kwa sasa katika matatizo makubwa ya kifedha, inaweza hata hivyo kufaidika kutokana na bei ya ununuzi chini ya viwango vya sasa: chini ya senti 10 za euro kwa kilowati saa, ikilinganishwa na karibu senti 30 leo. Matarajio ambayo yanaweza kusaidia kurweka sawa akaunti za kampuni.
Ili kuwahakikishia wawekezaji, Benki ya Maendeleo ya Afrika imekubali kuwa mdhamini endapo Jirama itakosa kulipa malipo yake. Ahadi muhimu ambayo inapaswa kuwahakikishia wawekezaji.
Wakati huo huo, mwito wa zabuni za ujenzi wa bwawa hilo ulifungwa wiki hii. Kampuni tatu ziko mbioni: moja ya Kichina, moja ya Kituruki na moja ya Ureno. Mazungumzo yataanza katika wiki zijazo, huku uamuzi ukitarajiwa mwishoni mwa mwaka.
Nyuma ya matukio, wale wanaohusika katika mradi huo wanatarajia kuanza kwa ufanisi wa kazi katika nusu ya pili ya mwaka 2026 – mradi ujenzi wa barabara ya kufikia, ambapo ilianza hivi karibuni, inaendelea bila mtengano.