
Emmanuel Macron amewasili Antananarivo, mji mkuu wa Madagascar leo Jumatano, Aprili 23, kwa ziara kiserikali ya siku mbili. Baada ya Mayotte na Réunion, raiswa Ufaransa anamalizia ziara yake katika viiwa vya Bahari ya Hindi nchini Madagascar. Zaidi ya mazungumzo baina ya nchi hizo mbili kuendeleza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, changamoto kwa Emmanuel Macron ni kuthibitisha jukumu la Ufaransa katika Bahari ya Hindi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu maalum huko Antananarivo, Valérie Gas
Emmanuel Macron amewasili nchini Madagascar akiwa na nia ya wazi: kuongeza ushawishi wa Ufaransa katika Bahari ya Hindi ili kuendelea kuendeleza mkakati wake wa Indo-Pacifiki. Ametoa hoja hiyo yake kabla ya kuondoka Réunion. “Katika eneo la Indo-Pasifiki, tuna zaidi ya wanajeshi 8,000. Hili ni jambo ambalo tulitarajia na kuliendeleza. Hii ndiyo sababu pia nimetaka kuwapo kwenye Tume ya Bahari ya Hindi nchini Madagascar, ambapo nitatetea nafasi ya Ufaransa na maeneo yake katika mazoezi ya pamoja, kwa ushirikiano wa kikanda, iwe inahusu chakula, elimu, hali ya hewa au usalama wa kiuchumi,” amesema Emmanuel Macron.
Ufaransa inajionyesha kama taifa lenye nguvu katika eneo hilo na kwa hivyo inatarajia kuwa na njia za kuifanya Mayotte kustahiki programu za Tume ya Bahari ya Hindi licha ya upinzani wa Comoro. “Kwa kweli kuna kutoelewana, hali ambayo tunafahamu, lakini tunaweza kushughulikia kwa heshima na, juu ya yote, kwa umakini zaidi,” rais wa Ufaransa amesema.
Changamoto pia ni za kiuchumi. Emmanuel Macron anaona Bahari ya Hindi kuwa soko kuu. “Ni soko, angalau la IOC, hata kwa upana zaidi, ambalo ni lazima tushinde. Afrika Mashariki… Bahari ya Hindi, pamoja na mitandao yake inayoenda hadi India kwenye baadhi ya sekta… Tunabadilisha ulimwengu,” amesema.
Katika mtazamo wake, Emmanuel Macron anatarajia kupata uungwaji mkono wa Madagascar.