Macron na Mahmud Abbas wa Palestine wasisitiza usitishwaji wa vita Gaza

Rais wa Palestina Mahmud Abbas na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron, wametaka usitishwaji wa haraka wa vita vinavyoendelea kwenye ukanda wa Gaza.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wito huu wa pamoja, umekuja baada ya mazungumzo ya simu kati ya viongozi hao wawili, ambao pia wanataka misaada ya kibinadamu  kuruhusiwa kuwafikia haraka Wapalestina, wanaoendelea kukabiliwa na vita kwenye ukanda wa Gaza.

Aidha, viongozi hao wamekataa pendekezo lolote la kuwahamisha wakaazi wa Gaza kutoka kwenye makaazi yao, wakati huu wanapoendelea kushuhudia mashambulio mazito kutoka kwa wanajeshi wa Israeli.

Siku ya Jumatatu, jeshi la Israeli limeendeleza mashambulio mazito ya angani, kulenga maeneo ya Khan Younis, Kusini mwa Gaza na kusababisha maafa.

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Mambo ya nje ya Palestina, imelaani matamshi ya Israel, baada ya rais Macron kusema kuwa Ufaransa inaweza kulitambua taifa huru la Palestina.

Kauli hiyo ya Macron ilishtumiwa vikali na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye alisema wazo la kiongozi huyo wa Ufaransa halipaswi kufikiriwa, kwa sababu wazo hilo linalenga kuharibu taifa la Israeli na kwa kuchukua ardhi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *