
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron leo Jumatano kwamba kuanza tena kwa mashambulio ya Israeli huko Gaza ni “hatua kubwa inayorudisha mambo nyuma,” na akaonya kwamba “hakutakuwa na suluhisho la kijeshi” katika ardhi ya Palestina.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Uhasama lazima usitishwe mara moja na mazungumzo lazima yaanze tena kwa nia njema chini ya mwamvuli wa Marekani,” amesema rais wa Ufaransa pamoja na Mfalme wa Jordan Abdullah II, aliyepokelewa katika Ikulu ya Elysée.
“Tunatoa wito wa usisitihwaji mapigano na kuachiliwa kwa mateka wote” wanaoshikiliwa na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza, ameongeza.
Kurejeshwa kwa mashambulizi ya Israel huko Gaza ni ‘hatua ya hatari sana,’ anasema mfalme wa Jordan
Kurejeshwa kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza ni “hatua hatari sana” ambayo inaongeza “watu kukata tamaa kwa hali mbaya ya kibinadamu,” Mfalme Abdullah II wa Jordan amelaani siku ya Jumatano alipowasili katika ikulu ya Élysée kwa ajili ya mkutano na Emmanuel Macron.
Mfalme Abdullah II ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua “mara moja” kwa ajili ya “kurejeshwa kwa usitishaji vita” na kuanza tena kwa misaada ya kimataifa, akilaani hatua ya Israel ya “kuzuia” usambazaji wa maji na umeme ambao “unahatarisha maisha ya watu walio hatarini zaidi.”