Mabao 10 ya Msuva na maana yake

MABAO 10 aliyofunga mshambuliaji wa Kitanzania, Simon Msuva kwenye klabu ya Al Talaba yameifanya timu hiyo kusalia nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Hadi sasa Ligi ya Iraq zimebaki mechi tano kumaliza msimu 2024/25, chama la Mtanzania huyo likiwa nafasi ya nne kwenye mechi 27, baada ya kushinda mechi 14, sare tano na kupoteza nane likikusanya pointi 47.

Kati ya pointi 47 hizo, Msuva pekee amechangia pointi 26 kwenye mabao aliyoyafunga msimu huu.

Kama nyota huyo asingefunga mabao hayo kwenye mechi zilizoipa ushindi Al talaba ingekuwa na pointi 21 pekee.

Kwa pointi 21, Talaba ingekuwa nafasi ya 19 kati ya 20 zinazoshiriki ligi hiyo nafasi moja kutoka mkiani.

Baadhi ya mechi alizofunga Msuva Aprili 17 Talaba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Al Kahraba, Aprili 12 ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Al Karma na alifunga Aprili 03 Al Hudod 1-3, Machi 14 Newroz 1-3, Machi 09 Naft Al-Basra 2-0 akiweka kambani yote mawili. Mechi nyingine ni ya Januari 29 dhidi ya Karbala akifunga katika 2-0 na Januari 24 dhidi ya Al Naft wakishinda 0-1.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *