Wakati hali ya utulivu ikidaiwa kuonekana Jumapili ya wiki iliopita huko Kivu Kusini kufiuatia wito uliotolewa na viongozi wa SADC na EAC, mamia ya watu wamejitokeza huko Brussels Ubelgiji kuandamana kuiunga mkono DRC na kuutuhumu Umoja wa Ulaya kutochukua hatua zozote.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Licha ya mvua iliokuwa ikinyesha, waandamanaji walijitokeza katika eneo maharufu la Lumumba jijini Brusels wakielekea katika ofisi za taasisi za Umoja wa Ulaya wakieleza lengo la ni kuuutaka Umoja wa Ulaya kuwa na msimamo kuhusu Rwanda na kuitaka kufuta mkataba wa Umoja wa Ulaya na Rwanda kuhusu madini lakini pia kwenye ushirikiano wa kijeshi.
Waandamanaji hao wamesema kutishswa vita haitoshi, inabidi kufuatiliwa kwa karibu utekelezwaji wa usitishwaji huo maana wanaopoteza maisha asilimia kubwa ni binadamu wasiokuwa na hatia yoyote.

Kulingana na vyanzo mbalimbali jana Jumapili kumeshuhudiwa ukimya kwenye uwanja wa mapigano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu Kusini kufuatia wito uliotolewa baada ya kikao cha viongozi wa SADC na EAC jijini Dar es salaam Jumamosi.
Mawaziri wa Ulinzi wa mashirika hayo mawili watakutana ndani ya siku 5 ili kufuatilia utekelezaji wa usitishwaji mapigano.