KATIBU wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 24,2025 jijini Dodoma kuelekea Mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Conversion na utahudhuriwa na wajumbe wa mkutano Mkuu kutoka maeneo mbalimbali.

KATIBU wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuelekea Mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Conversion.
Na.Alex Sonna-DODOMA
MAANDALIZI kwa ajili ya mkutano Mkuu maalumu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa yamekamilika na unatarajiwa kufanyika Mei 29-30 katika ukumbi wa Jakaya Conversion na utahudhuriwa na wajumbe wa mkutano Mkuu kutoka maeneo mbalimbali.
Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, CPA Amos Makalla,ameyasema hayo leo Mei 24,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea Mkutano huo.
“Tunauhakika tutaweka historia ya kuwa na mkutano wa kipekee kuvunja historia ya ule uliopita,maandalizi yamekamilika hata nyie Waandishi mnaona ukumbi unaendelea kupambwa sisi kila siku tunataka kufanya mambo ya kihistoria,”amesema CPA Makalla.
Aidha amesema kuwa mkutano huo utatanguliwa na kikao cha kamati Kuu ambacho kitafanyika Mei 26 na kisha Halmashauri Kuu Mei 28 .
Katika hatua nyingine,Makalla amesema kuwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano,Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la Makao Makuu ya CCM Mei 28 mwaka huu.
Amesema kuwa Jengo hilo litakuwa la kisasa ambalo litakuwa na huduma zote muhimu na litaendana na hadhi ya CCM ambayo kwa sasa inawanachama zaidi ya milioni 11.
“Tunajenga jengo la Makao Makuu pembeni ya Jengo hili ( Jakaya Conversion) ambalo litakuwa na facilities zote CCM ni Chama kikubwa Tanzania pamoja na Afrika,tumeona umefika wakati wa kuwa na jengo lenye facilities zote kumbi za mkutano, parking kwa sababu Chama hichi ni kimbilio la wananchi,”amesema Makalla.
Aidha amesema kuwa mkutano huo utakuwa na agenda tatu ambazo ni kupokea taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano kwa Serikali zote mbili,uzinduzi wa ilani ya uchaguzi 2025-2030 na marekebisho madogo ya katiba.
“Nitumie fursa hii kuwaalika wajumbe wote wa mkutano Mkuu karibuni Dodoma mambo yote yamekamilika tunawakaribisha hata ambaye sio mwananchi hata kama hujaalikwa unakaribishwa pia tutaweka eneo maalumu kwa ajili ya kuangalia,”amesema
The post MAANDALIZI YA MKUTANO MAALUM CCM TAIFA YAIVA JIJINI DODOMA appeared first on Mzalendo.