London yazungumzia juu ya mazungumzo ‘yenye tija’ na Marekani juu ya makubaliano ya kiuchumi

Uingereza na Marekani ziko kwenye mazungumzo ya makubaliano ya kiuchumi ambayo yatawezesha London kukwepa ushuru wa Marekani. Katika mazungumzo ya simu, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Marekani Donald Trump wamekaribisha mazungumzo hayo kama “ya tija,” kulingana na Downing Street.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Na: RFI na mashirika mengine

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wamezungumza kwa njia ya simu siku ya Jumapili, Machi 30. Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Marekani Donald Trump wamejadili “mazungumzo yenye tija kati ya timu zao kuhusu mpango wa ustawi wa kiuchumi kati ya Uingereza na Marekani,” Downing Street imeripoti.

“Wamekubaliana kwamba mazungumzo haya yataendelea kwa kasi endelevu wiki hii,” taarifa ya Downing Street imesema.

Tangu Londo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, kuanzia Januari 1, 2021, imekuwa ikitazamia makubaliano ya kibiashara na mshirika wake mkuu, ambayo yangeiwezesha kuepuka ushuru wa forodha wa Marekani unaolenga nchi nyingi za Ulaya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *