London, England. Liverpool imezidi kuukaribia Ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Everton katika mchezo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Anfield.
Ushindi ilioupata Liverpool unafanya ifikishe jumla ya pointi 73 ikiwa katika kilele cha Ligi Kuu England kwa tofauti ya pointi 12 mbele ya Arsenal inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 61.
Katika mchezo wa jana, bao pekee la Liverpool lilifungwa na Diogo Jota dakika ya 57 akiitumia vyema pasi ya Luis Diaz.

Hadi sasa Liverpool imeshinda jumla ya mechi 22 za Ligi Kuu, imetoa sare mechi saba na kupoteza mechi moja katika michezo 30, ambayo imecheza huku ikifunga jumla ya mabao 70.
Liverpool imebakiza michezo nane kuitimisha msimu wa Ligi Kuu England huku ikihitaji pointi 13 ili kutangazwa kuwa mabingwa wa EPL msimu huu.
Majogoo hao wa Jiji la London wanatakiwa kushinda mechi nne na kupata sare mechi moja. Hata hivyo, idadi ya pointi 13 zinaweza kupungua endapo Arsenal inayoshika nafasi ya pili itapoteza au kutoa sare kwenye mechi zake zilizobakia.
Katika michezo nane iliyobakiza, Liverpool itakutana na Fulham, West Ham, Leicester City, Tottenham, Chelsea, Arsenal, Brighton na Crystal Palace.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa jana:
Brighton 0 – 3 Aston Villa
Newcastle 2 – 1 Brentford
Man City 2 – 0 Leicester City
Southampton 1 – 1 Crystal Palace
Bournemouth 1 – 2 Ipswitch Town.