‘Live performance’ ipo salama kwa mastaa hawa

Dar es Salaam. Kwenye moja ya mijadala ya kiburudani inayoendelea kutrendi mitandaoni ni kuhusiana na ishu ya kuimba live baina ya mtayarishaji wa zamani wa muziki, Master Jay ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Sanaa (BASATA) akimtaja Ali Kiba hajui kuimba live.

Unaweza kujiuliza kwa nini Live hiyo ni sanaa inayohusisha msanii kuimba moja kwa moja mbele ya hadhira bila kutumia kurekodiwa awali, tofauti na playback, ambapo msanii anaiga sauti yake iliyorekodiwa.

Live Performance ni uimbaji wa moja kwa moja ambao unamuonyesha msanii uwezo wake wa kuimba na jukwaa kuendana na ala za muziki.

Faida za kuimba live zinasaidia kuboresha uwezo wa msanii kimuziki, kuongeza ubunifu wa kisanii, na kuimarisha uhusiano wa moja kwa moja kati ya msanii na hadhira.

Pia, uimbaji wa live huchangia katika kukuza heshima ya msanii, kupanua nafasi za ajira kwa wanamuziki wa moja kwa moja kama vile wapiga vyombo, na kuleta burudani halisi yenye hisia tofauti na ile msanii anayerekodi studio.

Baadhi ya wasanii wamekuwa wakikwepa kuimba live na hilo linatokana na hofu ya jukwaa, wengine wanakwepa gharama kubwa kwa sababu kwani onyesho litahitaji bendi ya muziki, mafundi wa sauti na vifaa maalum.

Sababu kubwa wasanii wengi hawafanyi mazoezi, kuimba live kunahitaji mazoezi makali ili kuboresha sauti, pumzi, na uwasilishaji kwa jumla na baadhi wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo.

Duniani kuna baadhi ya mifano ya mastaa, Beyonce ana uwezo wa kufanya vitu vingi anapokuwa jukwaani, Adele, Bruno Mars, Chris Brown ambaye pamoja na kucheza bado ana uwezo mzuri wa kuimba live.

Kwa Afrika wasanii kama Burna Boy wa Nigeria mmoja wa mastaa wanaofanya vizuri na mara kadhaa hutumia bendi yake (The Outsiders) kuburudisha jamii, Yemi Alade ni moja wa wanadada wanaofanya vizuri Afrika na sio tu kupafomu live lakini baadhi ya ngoma zake huziimba live na kuziposti Youtube.

Mwanaspoti limekuchambulia baadhi ya mastaa wa Tanzania ambao ni wakali wa kuburudisha kwa live.

Huyu ni habari nyingine kwenye kuimba live.Hajatoa ngoma muda mrefu lakini ni kipaji kingine ambacho mashabiki wengi walitamani nyota huyo kufka mbali.

Kwa sasa anaonekana kwenye moja ya kanisa hapa Dar es Salaam ambalo inadaiwa anafanya ibada hapo na mara kadhaa anaimba live.

Achana na sauti yake inayowadatisha mashabiki wengi lakini kinachovutia zaidi kwake ni uwezo wa kucheza na ala za muziki anapokuwa anaimba live.

Alipita T.H.T miongoni mwa vyuo vya muziki vilivyozalisha vipaji vingi hapa nchini waliopita mastaa kama Nandy, Maua Sama, Jay Melody, Barnaba na wengineo.

Rejea kwenye ukurasa wa Coke Studio Africa, miaka nane iliyopita mwanadada huyo akiimba live wimbo wa Forever na wasanii Nyanshinski wa Kenya na Yemi Alade na kuwainua baadhi ya mashabiki kwa sauti yake.

Mwaka jana alishinda tuzo ya albamu bora ya mwaka 2023 tuzo zilizotolewa na TMA na albamu yake ‘Love Sound Different’ ndani ya albamu hiyo aliwashirikisha wasanii Diamond, Nandy, Jux, Marioo na wengineo.

Hata hivyo tuzo hiyo baadae alimkabidhi Marioo ambaye alilalamika mitandao kuwa tuzo hizo hazikutendewa haki akiamini alistahili kupewa.

Mara kadhaa amekuwa akipafomu kwenye mikutano mbalimbali ile ya Chama cha Mapinduzi akiimba live na bendi jambo linalompa thamani kwenye karia yake ya muziki.

Ni fundi haswa wa kucheza na ala za muziki anapokuwa jukwaani kitendo ambacho kinawafanya baadhi ya mashabiki kummwagia sifa zake juu ya uwezo huo.

Ni mmoja wa wasanii waliopita kwenye mashindano ya kutafuta vipaji kwa wanamuziki wa Bongo Star Search alikopita mastaa kama Harmonize, Asagwile, Kayumba na wengineo.

Kwa kuthibitisha kwamba anaweza kuimba live performance kipimo sahihi ni yale mashindano ambayo kuna hatua ikifika mshiriki anapaswa kuimba live akiwa na bendi lengo ni kupima uwezo wake wa kuimba, kuendana na Key na pumzi.

Hata hivyo Phina alifanikiwa kupita huko kote na baadae kuibuka mshindi mbele ya majaji, Salama Jabir, Master Jay na Rita Paulsen.

Phina kwa sasa anatamba na wimbo wa ‘Romeo and Julieth’ aliomshirikisha msanii kutoka nchini Kenya, Otile Brown wiki tatu zilizopita.

Upo Nyonyo, Sisi ni Wale, TiTiTi ni miongoni mwa ngoma alizozifanya zikapata mapokezi makubwa kwa mashabiki ambao wanafananisha sauti yake na Vanessa Mdee.

Hajapitia mikiki kwenye muziki wake kwani ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wana uwezo wa kupiga ala za muziki kama gitaa, Piano na Viollin.

Alianza sanaa ya uimbaji tangu akiwa na miaka mitano akiwa shuleni na kujifunza kupiga vyombo vya muziki.

Kazi yake ya kwanza iliyompa umaarufu mkubwa ilikuwa ‘Super Woman’ ambayo ndani yake waliimba mastaa kibao wa kike akiwemo Zuchu, Ruby na LuluDiva kwenye kilele cha siku ya wanawake duniani.

Baada ya kazi hiyo ambayo alipewa mashavu na Diamond Platnumz ambaye ndio alikuwa akisimamia wimbo huo tangu studio hadi kushuti video ilionekana kuwakosha baadhi ya wasanii hasa kwenye kile kipande cha kupiga Viollin.

Awali nyota huyo aliyesainiwa na lebo ya Sony Music alikuwa akiimba nyimbo za injili lakini baadae upepo ukabadilika na kuanza kuimba Bongo Fleva.

Ngoma yake ya kwanza ilikuwa ‘Tucheze’aliyoitoa miaka mitatu iliyopita iliyowafanya mashabiki mumpa sikio na kuanza kumsikiliza hadi sasa akitajwa miongoni mwa wasanii chipukizi watakaoleta mapinduzi kimataifa.

Ukiwataja mafundi wa kuimba live basi jina la Ali Kiba halikosekani kwenye orodha hiyo, Mkurugenzi huyo wa lebo ya ‘King Music’.

Hivi karibuni Prodyuza wa zamani wa BongoFleva, MasterJay alimtaja msanii huyo mkongwe kuwa hajui kuimba live, ishu iliyozua mijadala mbalimbali mitandaoni.

Wapo baadhi ya mashabiki waliosema Prodyuza huyo alikosea kumzungumzia vile Kiba ambaye ni mshindani mkubwa wa Diamond hapa nchini na wengine walimuunga mkono.

Miaka nane iliyopita Ali Kiba alikuwa mmoja wa wasanii waliopafomu kwenye jukwaa kubwa la muziki, MTV Africa Music Awards na kundi la Kenya SautSol wakiimba wimbo wa pamoja ‘Unconditionally Bae’ ambao walishirikiana.

Hata hivyo, ni mmoja wa wasanii ambao wanapopata nafasi ya kutumbuiza hutumia ala za muziki akionyesha ufundi wake wa kuimba bila biti ya muziki waliourekodi.

Alianza kama masihara safari yake ya muziki pale rafiki yake alipomtambulisha kwa Ruge Mutahaba aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania House of Talent (THT), hapo akatengenezwa na wimbo wake wa kwanza Nagusagusa ulipata umaarufu mkubwa mara tu baada ya kuachiwa.

Mwishoni mwa mwaka 2015 alishiriki mashindano ya ‘Tecno Own the Stage’ lililoshirikisha karibu mastaa kutoka bara la Afrika lakini mwanadada huyo alipenya.

Katika fainali hiyo iliyofanyika Lagos nchini Nigeria, Nandy aliibuka mshindi wa pili mbele ya majaji wakati huo, Yemi Alade wa Nigeria, Bien wa Sautsol nchini Kenya na M.I Abaga.

Hakukawia mwaka 2017 akatoa wimbo ‘One Day’ ambao ulifanya vizuri na kufanya baadhi ya wapenda muziki kuanza kumfuatilia.

Kutokana na ujuzi wake mwaka huo huo alipata nafasi ya

kushiriki Coke Studio Africa ambapo alipafomu nyimbo mbalimbali, aliteuliwa kuwa na kuibuka mshindi wa tuzo za All Africa Music Awards kama msanii bora wa kike kutoka Afrika Mashariki. 

Kitendo cha kuibuka mshindi wa pili mbele ya majaji ambao ambao wanafanya vizuri kwenye tasnia hiyo Afrika kulimpa uwezo zaidi mwanadada huyo ambaye anamiliki lebo ya ‘The African Princess’ akimsaini msanii mmoja Yammi.

Kwa sasa hayuko kwenye lebo ya Wasafi akiachana nayo hivi karibuni huku sababu za kuondoka kwake zikiwa hazijajulikana.

Mbosso anakuwa msanii wa nne kuondoka ndani ya lebo hiyo chini Diamond baada ya Rich Mavoko, Harmonize, Rayvanny ambao walipotoka wakaanzisha lebo zao na kila mmoja akimiliki msanii mmoja.

Msanii huyo ambaye anasifika kwa utunzi wa nyimbo za mapenzi kwa sasa na wimbo wa Kupendwa ambao ndani ya mwezi mmoja umeingiza zaidi ya watazamaji Milioni 3.

Ni mmoja wa wasanii wa zamani waliounda kundi la Yamoto Band akiwa na Beka Flavour, Aslay na Enock Bella ambapo baadae kundi hilo lilivunjika na kila mtu alifata njia yake.

Ngoma kama Cheza kwa Madoido, Nitakupwelepweta, Mpaka Nizikwe, Niseme na nyinginezo ni miongoni mwa nyimbo zilizowapa umaarufu mkubwa wasanii hao.

Linapokuja suala la kuimba bila ya biti, Mbosso ni habari nyingine kwani sauti yake ambayo anaimba mahadhi ya Pwani imekuwa ikiwaburudisha mashabiki zake.

Lady Jaydee 

Licha ya umri wake kwenda akiwa miongoni mwa wanawake wa muda mrefu waliodumu kwenye gemu ya muziki, Lady Jaydee ni mkali anapoimba live.

Ni wasanii wachache waliodumu kwenye Bongo Fleva ambao wana uwezo mkubwa wa kupafomu na mara kadhaa amekuwa akiimba kwenye matamasha mbalimbali.

Diamond Platnumz

Diamond ni mmoja wa wasanii wanaotajwa kwa Afrika kuwa na mafanikio makubwa hasa kwenye soko la kimataifa akifanya kolabo na wasanii wakubwa duniani.

Ngoma ya Komasava aliyomshirikisha Jason Derulo na Chley, Khalil Harisson kutoka Afrika Kusini ambayo hadi sasa inafanya vizuri Youtube ikiwa na watazamaji Milioni 41 ndani ya miezi saba imemfanya aendelee kufuatiliwa zaidi.

Mara kadhaa amekuwa akiimba na bendi kuonyesha uwezo wake wa sauti, ameshaimba kwenye matamasha makubwa kama MTV Base Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *