Libya, Sudan zinaongoza ajenda ya vikao vya Baraza la Amani Usalama la Afrika

Migogoro ya Libya na Sudan imetawala siku ya tatu ya vikao vya kabla ta mkutano wa kilele wa viongozi wa Afrika katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, huku makao makuu ya Umoja wa Afrika yakitarajiwa kuandaa hafla ya kutiwa saini mkataba wa maridhiano kati ya pande zinazohusika katika mgogoro wa Libya.