Libya: Mchakato wa kufufua uhusiano kati ya Benghazi na Minsk unaendelea

Ujumbe wa ngazi ya juu wa Belarus ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu Viktor Karankevich na unaojumuisha mawaziri sita umehitimisha ziara ya siku mbili huko Benghazi mashariki mwa Libya, chini ya udhibiti wa Marshal Khalifa Haftar, siku ya Jumatatu, Machi 10. Mikataba sita ya mfumo ilitiwa saini na serikali ya Osama Hamad. Na hii, katika nyanja za afya, kilimo, viwanda na mafuta. Ujumbe huo pia ulijumuisha maafisa wa idara za ujasusi za Minsk.

Imechapishwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya serikali ya Osama Hamad imeeleza kuwa ziara hiyo ni sehemu ya “kuimarika kwa uhusiano katika nyanja mbalimbali kati ya nchi hizo mbili marafiki.” Inalenga “kuinua kiwango cha ushirikiano wa pamoja.” Kwa hakika, ujumbe wa Belarus umefanya mikutano mingi ya kiuchumi mjini Benghazi, hususan katika sekta ya mafuta, ambako ulitia saini mikataba ya utafiti wa gesi na mafuta mashariki na kusini mwa Libya, siku chache baada ya serikali ya Tripoli kutangaza kuwa inafungua zabuni ya sekta ya mafuta kwa makampuni ya kigeni.

Hata hivyo, uwepo wa mkuu wa idara ya ujasusi ya Belarusi huko Benghazi, pamoja na ujumbe wa kisiasa na kiuchumi wa nchi yake, unaonyesha kuwa sehemu iliyo siri zaidi ya ziara hiyo inahusu masuala ya usalama na kijeshi, waangalizi wanabainisha. Ziara hii ya ujumbe wa Belarus nchini Libya unakuja chini ya siku ishirini baada ya ziara ya Marshal Haftar huko Minsk na mkutano wake na Rais Lukasjenko. Rais Lukasjenko alibainisha kwamba atamsaidia na makubaliano ya kijeshi yaliripotiwa kutiwa saini kutoa mafunzo kwa maafisa wa Jeshi la Kitaifa la Libya (LNA) huko Minsk.

Hata hivyo, mkutano ulifanyika Benghazi kati ya Waziri wa Ulinzi wa Belarus na Saddam Khalifa Haftar katika nafasi yake kama kamanda wa vikosi vya ardhini vya LNA. Serikali ya mashariki mwa Libya inaendelea na juhudi zake za kujiondoa katika kutengwa kimataifa. Benghazi inatafuta kufikia mataifa ambayo hayana maelewano mazuri na serikali ya Dbeibah mjini Tripoli.

Wachambuzi wa Libya wanaamini kuwa maelewano kati ya Benghazi na Minsk yameanzishwa na kutiwa moyo na Moscow, ambayo inataka kuongeza uwepo na ushawishi wake kijeshi na kiuchumi barani Afrika kupitia Libya. Kulingana na wao, Minsk ni sura tu ya mbele ya Moscow katika kuingilia kati katika kanda hii. Hili si jambo la kushangaza, kwani ziara ya wajumbe wa Belarus inalingana na uwepo wa Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi Yunus-bek Yevkurov, ambaye alionekana siku ya Ijumaa, Machi 7, huko Benghazi, akihudhuria ibada ya maombi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *