Liberia: Aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi Jonathan Fonati Koffa azuiliwa

Aliyekuwa Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Liberia, Jonathan Fonati Koffa, amezuiliwa katika makao makuu ya polisi ya taifa. Anashtakiwa pamoja na maafisa wengine kadhaa waliochaguliwa kwa kisa cha moto katika jengo la Congress mwezi wa Desemba mwaka uliyopita.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Matukio haya “yanahusu sana na yanakumbusha kisa kibaya kilichotokea katika historia ya taifa letu,” wapinzani kadhaa, ikiwa ni pamoja na rais wa zamani George Weah, wamesema. Wanataka Jonathan Fonati Koffa na wabunge wengine wanaohusishwa kuachiliwa huru bila masharti.

Jonathan Fonati Koffa ni mfuasi wa chama cha siasa cha rais huyo wa zamani. Kuendelea kwake kama Spika wa Bunge la Liberia kumezua mvutano wa miezi kadhaa.

Kama ukumbusho, mnamo mwezi Oktoba, karibu viongozi hamsini waliochaguliwa walipiga kura ya kushtakiwa kwake, wakimtuhumu kwa utawala mbovu na ufisadi. Walianza kufanya vikao vyao peke yao, vikiongozwa na spika wao wa Bunge, mfuasi wa chama cha rais wa sasa, Joseph Boakai.

Ushahidi thabiti, kwa mujibu wa mkuu wa polisi

Mivutano ya kisiasa inaongezeka. Mwezi Desemba, mji mkuu, Monrovia, ulikumbwa na maandamano ya kumuunga mkono Jonathan Fonati Koffa. Ni katika tukio hilo la maandamao ambapo moto mkali uliharibu jengo la Baraza la Congress mnamo Desemba 18.

Mnamo mwezi Aprili, Mahakama ya Juu iliamua kuunga mkono Jonathan Fonati Koffa, na kubatilisha kuondolewa kwake. Hata hivyo, aliamua kujiuzulu katikati ya mwezi Mei. Sasa anashtakiwa kwa “kuchoma moto, kuhatarisha wengine, na kujaribu kuua.”

Kulingana na mkuu wa polisi, kuna ushahidi thabiti dhidi yake. Upinzani unazungumza juu ya “ujanja hatari wa kisiasa” kwa utulivu wa nchi.

Abdullah Kiatamba (mtaalam wa masuala ya siasa nchini  Liberia)anasema serikali lazima ionyeshe kwamba ina ushahidi, na ushahidi huo lazima uwe thabiti.”

Ikiwa ushahidi sio wa kushawishi, haitakuwa wazo nzuri, kwani inaweza kutuma ujumbe usio sahihi. Tutaona majibu yanayofuata yatakuwaje. Upinzani bado unakutana. Ni mapema sana kusema kama kutakuwa na machafuko au la. Lakini kuna msururu mkubwa wa polisi kote nchini, haswa katika gereza ambalo Koffa na wabunge wengine wamefungwa. Kuna uwepo mkubwa wa polisi katika maeneo mengi ya jiji. Mvutano unaonekana, lakini hakuna vurugu iliyoshuhudiwa hadi sasa. Hakuna fujo kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *