Lebanon yanaunda serikali ya kwanza baada ya zaidi ya miaka miwili

Lebanon imeunda serikali yake ya kwanza kamili tangu mwaka 2022, wakati huu ambapo nchi hiyo ya Kiarabu inajitahidi kujenga upya eneo lake la kusini lililoharibiwa na vita; na kuhakikisha usalama unarejea baada ya mapigano kati ya Israeli na Harakati ya Muqawama ya Hizbullah.