Lavrov: Sera ya ‘Marekani Kwanza’ inatoa mwangwi wa kaulimbiu ya Hitler ya ‘Ujerumani iko juu ya wote’

Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov ametahadharisha kuwa, sera ya Marekani ya ‘Marekani Kwanza’ ina mfanano wa kutatanisha na kaulimbiu ‘Ujerumani iko juu ya wote’ iliyotumiwa na Wanazi kuthibitisha ukuu na kuwa bora kitaifa kuliko wengine.