Lavrov: Mkataba wa ushirikiano wa ulinzi kati ya Russia na Iran utatiwa saini hivi karibuni

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Russia ametangaza kuwa makubaliano ya ushirikiano wa pamoja wa ulinzi kati ya Moscow na Tehran yatatiwa saini hivi karibuni.

Sergei Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, amesisitiza kwamba, makubaliano yatakayotiwa saini hivi karibuni kati ya nchi yake na Iran yanajumuisha ushirikiano zaidi wa ulinzi.

Lavrov pia amesema kwamba kabla ya mwisho wa mwaka huu, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, atatembelea Moscow ili kutia saini makubaliano hayo ya ulinzi na Rais wa Shirikisho la Ruusia, Vladimir Putin.

Ikumbukwe kuwa, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alikwenda Kazan, Russia wiki iliyopita kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha nchi wanachama wa BRICS na kukutana na Rais wa Russia pambizoni mwa mkkutano huo.