Kwa nini marafiki zako wanakufanya uishi maisha marefu zaidi

tt

Chanzo cha picha, Getty Images

Watu unaotangamana nao maishani huathiri mwenendo wako wa kawaida kama vile mazoezi. David Robson, mwandishi wa kitabu kipya kuhusu mahusiano yetu, anaangazia uhusiano kati ya vitu hivi viwili.

Ikiwa umezingatia mawazo ya hivi punde juu ya ustawi na maisha marefu, utakuwa umeona kuongezeka kwa umakini katika hali ya mahusiano yetu. Watu walio na mitandao ya kijamii inayostawi, tunaambiwa, huwa na afya bora zaidi kuliko wale wanaohisi kutengwa.

Kutangamana kwetu kunahusishwa sana na maisha marefu hivi kwamba Shirika la Afya Ulimwenguni limeanzisha Tume mpya ya Uhusiano wa Kijamii, na kuiita “kipaumbele cha afya duniani”.

Huenda ukatilia shaka madai haya, na taratibu za ajabu ambazo zinapaswa kuunganisha ustawi wetu wa kimwili na nguvu ya mahusiano yetu. Lakini uelewa wetu wa mtindo wa “biopsychosocial” wa afya umekuwa ukikua kwa miongo kadhaa.

Nilipokuwa nikichunguza sayansi ya kitabu changu The Laws of Connection, niligundua kwamba urafiki wetu unaweza kuathiri kila kitu kuanzia nguvu ya mfumo wetu wa kinga hadi uwezekano wetu wa kufariki kutokana na ugonjwa wa moyo.

Pia unaweza kusoma:

Hitimisho la utafiti huu ni wazi: ikiwa tunataka kuishi maisha marefu na yenye afya, tunapaswa kuanza kuwapa kipaumbele watu wanaotuzunguka.

Mizizi ya sayansi inaweza kufuatiliwa hadi mwanzoni mwa miaka ya 1960. Hapo zamani, Lester Breslow katika Idara ya Afya ya Umma ya Jimbo la California alianzisha mradi kabambe wa kutambua tabia ambazo zilichangia ustawi na maisha marefu zaidi.

Ili kufanya hivyo, aliwajumuisha karibu washiriki 7,000 kutoka Kaunti inayozunguka Alameda. Kupitia dodoso za kina, aliunda taswira ya kina zaidi ya mitindo yao ya maisha, na kisha kufuatilia ustawi wao kwa miaka iliyofuata.

Utafiti kuhusu manufaa ya kiafya ya urafiki unaweza kufuatiliwa hadi miaka ya 1960 California

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Utafiti kuhusu manufaa ya kiafya ya urafiki unaweza kufuatiliwa hadi miaka ya 1960 California

Ndani ya muongo mmoja, timu ya Breslow ilikuwa imetambua viungo vingi ambavyo sasa tunajua ni muhimu kwa afya njema: usivute sigara; kunywa pombe kwa uangalifu; kulala saa saba hadi nane usiku; kufanya mazoezi; kuepuka vitafunio; kudumisha uzito wa wastani; kula kifungua kinywa.

Wakati huo, matokeo yalikuwa ya kushangaza kiasi kwamba wenzake walipomletea matokeo, aliamini walikuwa wakifanya mzaha. Hutaweza kuelezea miongozo hii kwa undani zaidi – “Alameda 7” sasa ndio msingi wa mwongozo mkuu wa afya ya umma.

Utafiti uliendelea, hata hivyo kufikia 1979, wenzake wawili wa Breslow – Lisa Berkman na S Leonard Syme – walikuwa wamegundua jambo la nane ambalo liliathiri maisha na ustawi wa watu: uhusiano wa kijamii.

Kwa wastani, watu walio na idadi kubwa ya mahusiano walikuwa karibu nusu ya uwezekano wa kufa kama watu ambao walikuwa na marafiki wachache.

Matokeo yalibakia hata baada ya kudhibiti mambo kama vile hali ya kijamii na kiuchumi na afya ya watu mwanzoni mwa utafiti, pamoja na matumizi ya sigara, mazoezi na lishe.

Ukweli wa mambo

Uhusiano wa kijamii unaweza kuongeza mfumo wako wa kinga na kukukinga kutokana na maambukizi, kwa mfano. Katika miaka ya 1990, Sheldon Cohen katika Chuo Kikuu cha Carnegie Mellon nchini Marekani aliwataka washiriki 276 kutoa maelezo kamili ya mahusiano yao ya kijamii.

Walijaribiwa kwa maambukizi yaliyopo, kisha wakawekwa karantini na kutakiwa kuvuta matone ya maji yaliyo na virusi vya rhinovirus – kirusi kinachosababisha kikohozi na na kumfanya mtu kupiga chafya sana.

Katika siku tano zilizofuata, wengi wa washiriki waliendelea kupata dalili, lakini hii ilikuwa na uwezekano mdogo sana ikiwa walikuwa na anuwai kubwa na tofauti ya miunganisho ya kijamii. Hakika, wale walio na viwango vya chini vya uhusiano wa kijamii walikuwa na hatari mara tatu hadi nne ya kueneza mafua kuliko wale walio na mtandao mkubwa wa familia, marafiki, wafanyakazi wenzao na marafiki.

Mwanasayansi yeyote mzuri anapaswa kuzingatia kila wakati ikiwa sababu zingine za kutatanisha zinaweza kuelezea matokeo.

Ni jambo la busara kudhani kuwa watu wapweke wanaweza kukosa kufaa na kufanya shughuli nyingi, kwa mfano, ikiwa wanatumia muda mchache kutangamana na marafiki na familia.

Berkman na Syme pia waligundua, kiungo hiki hata hivyo kilibakia hata baada ya watafiti kuzingatia mambo hayo yote. Na ukubwa wa athari unazidi kwa kiasi kikubwa manufaa ya kuongeza virutubisho vya vitamini – hatua nyingine tunaweza kuchukua ili kuimarisha mfumo wetu wa kinga.

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuimarika kwa afya ya jamii kunatuepusha na hatari ya kupata magonjwa sugu, yanayobadilisha maisha kama vile kisukari cha aina ya 2. Hii hutokea wakati kongosho inapoacha kutoa insulini ya kutosha, na seli za mwili huacha kuitikia insulini inayotiririka kupitia damu – zote mbili ambazo huizuia kugawanya sukari ya damu hadi seli zenye nguvu.

Mambo kama vile unene wa kupindukia yanaweza kuchangia ugonjwa wa kisukari, lakini ndivyo inavyoonekana, ubora wa mahusiano yako. Utafiti wa washiriki 4,000 katika Utafiti wa Uingereza wa Longitudinal wa Kuzeeka uligundua kuwa alama ya juu kwenye Kiwango cha Upweke cha UCLA – dodoso ambalo wanasayansi hutumia kupima uhusiano wa kijamii – lilitabiri mwanzo wa kisukari cha aina ya 2 katika muongo uliofuata. Kuna hata ishara kwamba watu walio na uhusiano thabiti wa kijamii wana hatari iliyopunguzwa ya kupata ugonjwa wa Alzheimer’s na aina zingine za shida ya akili.

Ushahidi hata hivyo, unahusu magonjwa ya moyo na mishipa. Tafiti kubwa zinazofuatilia afya ya maelfu ya watu kwa miaka mingi zimeangazia kiunga hicho mara kwa mara.

Hii inaweza kuonekana katika hatua za mwanzo – watu walio na uhusiano mbaya wa kijamii wana uwezekano mkubwa wa kuendeleza shinikizo la damu – na katika matokeo mabaya zaidi, na upweke huongeza hatari ya mashambulizi ya moyo, angina au kiharusi kwa karibu 30%.

Ili kupata kipimo cha umuhimu wa jumla wa kukuza afya ya jamii, Julianne Holt-Lunstad, mwanasaikolojia katika Chuo Kikuu cha Brigham Young, huko Provo, Utah, alikusanya matokeo ya tafiti 148.

Kwa pamoja walishughulikia washiriki 300,000 na walikuwa wameangalia faida za ushirikiano wa kijamii na hatari ya kukatwa kwa jamii. Kisha akalinganisha madhara ya upweke na hatari za mambo mengine mbalimbali ya mtindo wa maisha, kutia ndani kuvuta sigara, kunywa pombe, mazoezi na mazoezi ya viungo, fahirisi ya uzito wa mwili (kipimo cha unene uliokithiri), uchafuzi wa hewa na kutumia dawa za kudhibiti shinikizo la damu.

Matokeo, yaliyochapishwa mwaka wa 2010, yalikuwa ya kustaajabisha: Holt-Lunstad iligundua kuwa ukubwa na ubora wa mahusiano ya kijamii ya watu yalilingana au yalizidi karibu mambo mengine yote katika kubainisha vifo vya watu.

Kadiri watu wanavyohisi kupendwa na watu wanaowazunguka, ndivyo afya zao zinavyoboreka na ndivyo uwezekano wao wa kufa mapema unavyopungua.

Soma pia:

Imetafsiriwana Ambia Hirsi