

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwishoni mwa Oktoba 2022, wataalamu wa magonjwa ya mlipuko na wataalam wa magonjwa ya kuambukiza kote ulimwenguni walianza kugundua mwelekeo usio na utulivu. Kama mtaalam wa magonjwa ya milipuko Adam Kucharski alivyoelezea kwenye Twitter, kulikuwa na wimbi jipya la Covid-19 lililoendelea – lakini lilikuwa likienda bila kutambuliwa.
Leo mienendo ya kutisha ya vifo vya Covid-19 na kulazwa hospitalini, ambayo sote tulikuwa tumeizoea wakati wa siku mbaya za 2020 na 2021, imebadilishwa na mfululizo wa visa zaidi, lakini usio na mwisho wa vifo vya kila siku.
Kwa mfano, hebu tuchukue takwimu za vifo 133 vinavyohusiana na Covid-19 vya 21 Desemba 2022 nchini Uingereza kulingana na tovuti ya serikali ya Uingereza – idadi ambayo inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza ikilinganishwa na 2020 wakati watu walikuwa wakifariki kwa maelfu kutokana na virusi (katika wiki hiyo hiyo nchini Marekani watu 2,919 walikufa kutokana na Covid-19).
Lakini kama Kucharski anavyoonyesha, baada ya muda hata viwango vya chini vya vifo vinaweza kuukua hadi kufikia idadi ya kushangaza, labda hata ya kushtua.
Katika mwaka mzima wa 2022, taarifa hiyo hiyo inaonyesha kuwa watu 46,099 walikuwa wameangamia kutokana na Covid-19 nchini Uingereza – serikali hairekodi tena data hii kwa Uingereza nzima.
Hii sio vifo 75,240 vilivyotokea mwaka 2020 au 74,558 au mnamo 2021, lakini bado ni zaidi ya vile ambavyo wengi wanaweza kutarajia. Kinyume chake, katika kipindi cha msimu mbaya wa homa ya mafua, karibu watu 30,000 nchini Uingereza wanaweza kufa kutokana na mafua na nimonia.
Ni vigumu sana kulinganisha data kati ya nchi na nchi katika ngazi ya kimataifa, kwa kuwa njia na vigezo vya kushughulikia covid imetofautiana sana.
Hata hivyo, WHO inakusanya idadi ya vifo vya Covid kama ilivyoripotiwa na nchi moja moja. Kutoka kwa hili tunaweza kujua ukubwa wa janga hili: mnamo mwaka 2022, zaidi ya vifo 1,215,000 vya Covid viliripotiwa kote ulimwenguni.
Idadi hii ni ya chini sana kuliko vifo 3,505,000 walioripotiwa mwaka uliopita, lakini bado ni idadi kubwa ya vifo – na kuna uwezekano kuwa zaidi ya hiyo kubwa kwa idadi halisi ya vifo.
Bado ndani ya maeneo mengi ya mamlaka – na hata vyumba vya habari – kote ulimwenguni, vifo hivi vinavyoendelea havitajwi ikilinganishwa na mambo mengine, ikiwemo vita, gharama ya maisha hadi bili za nishati. Bado kote ulimwenguni, Covid-19 imekuwa ikitoweka kwa miezi kadhaa.
‘Uchovu wa Virusi wa Corona’
Wanasayansi wanakubali kwamba inaweza kuchukua muda, kama vile kutokea kwa athari kubwa zaidi , kwa hili kubadilika. Au, kama Kucharski anavyosema, tumezingatia sana hatua ya mwisho linapokuja suala la vifo vinavyohusiana na Covid, tumepuuza jinsi idadi hii ya vifo inayoenea bado inaweza kuongeza na kuwa idadi kubwa sana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hali kama hiyo imeonekana nchini Marekani, ambapo Wamarekani 2,000-3,000 bado wanakufa kutoka kwa Covid-19 kila wiki. Mtaalamu wa magonjwa wa Chuo Kikuu cha Harvard William Hanage anasema kwamba aliwaandikia waandishi wa habari katika shirika moja kubwa la vyombo vya habari Julai mwaka jana, akiwafahamisha kwamba ikiwa idadi ya vifo vinavyoendelea vya kila juma itaongezwa hadi mwaka mzima, itakuwa sawa na misimu mitatu ya homa mbaya hasa.
Lakini habari kama hizo hazipewi kipaumbele na vyombo vya habari. “Idadi ni kubwa sana,” anasema Hanage. “Lakini moja ya mambo ambayo hutokea kwa wanadamu ni kwamba mambo ambayo hutokea mara kwa mara kila siku huwa sehemu ya maisha yetu na tunayazoea.” “Tumekuja kuzingatia sana wakati kuna miiba mikubwa,” anasema Denis Nash, mtaalam wa magonjwa katika Chuo Kikuu cha Jiji la New York.
“Hiyo imetengeneza hali ambayo watu sasa hawazingatiaa kile kinachoweza kutokea. Lakini unapoanza kuiangalia baada ya muda, inatisha ni vifo vingapi vinavyotokea leo. .”
Kwa Nash na wengine, moja ya vitu vinavyofadhaika ni kwamba vifo hivi vingi vinaweza kuzuilika.
Chanjo ya kwanza na ile ya nyongeza
Nyuma ya grafu na taswira zisizo na mwisho kwenye tovuti za serikali, ni jambo la kushangaza kuwa ni vigumu kupata takwimu ili kuelewa kikamilifu ni kina nani bado wanakufa kutokana na Covid-19.

Chanzo cha picha, Getty Images
Simulizi za vifo hivi unawea kupata kwa uhalisia kwa kuzungumza na madaktari walio mstari wa mbele hospitalini. Kulingana na William Schaffner, profesa wa magonjwa ya kuambukiza katika Kituo cha Matibabu cha Chuo Kikuu cha Vanderbilt huko Nashville, Tennessee, wanaokufa ni bado ni wale ambao walikuwa hatarini zaidi katika siku za mwanzo za janga hilo.
“Watu tunaowaona wamelazwa hospitalini huwa ni wale ambao ni wazee, au vijana ambao wana kinga dhaifu, iwe kwa sababu ya ugonjwa au dawa ambayo inadhoofisha mfumo wao wa kinga,” anasema Schaffner.
“Ni makundi mengi ya hatari.” Andrew Ustianowski, mshauri katika Hospitali Kuu ya Manchester Kaskazini ya Uingereza, anauga mkono. “Vifo ambavyo ningeweza kufikiria kuwa nimehusika hivi majuzi vimekuwa vya watu ambao kwa kiasi kikubwa wamepungukiwa na kinga au dhaifu sana, na kwa hivyo Covid ina athari kubwa,” anasema. “
Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa jumla ya watu milioni 26 nchini Uingereza wanastahili kupata chanjo ya nyongeza ya Covid 19, lakini ni nusu tu kati yao wamechapata chanjo hiyo hadi sasa.
Kusitasita au kusuasua kupokea chanjo ya nyongeza kunahusu zaidi Marekani, huku 29.6% tu ya Wamarekani wenye umri wa zaidi ya miaka 65 walipata dozi zao za chanjo hivi karibuni.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulinda walio hatarini
Kwa sababu athari inayoendelea ya Covid-19 inawagusa zaidi walio hatarini zaidi, maswali yanaulizwa ikiwa jamii kwa ujumla juhudi zinapaswa kufanywa zaidi kuwalinda, na kutafuta njia za kupunguza idadi inayoendelea ya vifo.
Ikiwa chanjo za ziada zingetolewa kwa makundi yote ya umri badala ya walio hatarini zaidi, zingeweza kuleta mabadiliko kwa kupunguza maambukizi, na usambazaji wa dawa za kuzuia virusi kama vile Paxlovid, ambazo zimetajwa kupunguza vifo.
Pia kuna hofu kwamba kingamwili za monokloni – protini zilizokuzwa kwenye maabara ambazo huongeza kinga ya mwili – kama vile Regeneron’s Regen-Cov na Astrazeneca’s antibody cocktail Evusheld, ambazo zimetajwa kuokoa maisha ya watu wengi walio na kinga dhaifu, zinapungua kwa kasi ufanisi wake.
Kama matokeo, Hanage anasema mbadala kama vile BQ 1.1 – inaweza kuwa na athari ndogo kwa watu, vinaweza kuchangia katika idadi ya vifo inayoendelea miongoni mwa walio hatarini zaidi.
“Inaonekana wazi kuwa matibabu ya antibody ya monoclonal kwa watu wanaohitaji hayatakuwa na ufanisi,” anasema. “Na maana yake ni kwamba baadhi ya watu walio katika mazingira magumu zaidi watakuwa na uwezekano mkubwa wa kung’ang’ana na maambukizi ya virusi ambavyo tutaviona wakati wa majira ya baridi kali.