Kwa nini Araqchi ametaja matamshi ya Guterres kuhusu Iran kuwa ni ya kifidhuli?

Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema akijibu hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu miradi ya nyuklia ya Iran kwamba: “Kufungamana kwa muda mrefu Iran na mfumo wa kimataifa wa kutoeneza silaha za maangamizi kuko wazi kwa kila mtu.”