
Harakatii ya Mapambano ya Hizbullah ya Lebanon kwa mara ya kwanza imekishambulia kwa makombora kituo cha ufuatiliaji wa kiufundi na kielektroniki cha utawala ghasibu wa Israel katika eneo la Golan linalokaliwa kwa mabavu.
Harakati ya muqawama ya Hizbullah jana mbali na kukishambulia kwa makombora kituo cha ufuatiliaji wa kiufundi na kielektroniki cha utawala wa Kizayuni (Oital) katika eneo la Golan inayokaliwa kwa mabavu, kwa mara ya kwanza ililipiga jengo moja katika mji wa al-Mutla, kaskazini mwa ardhi zinazokaliwa kwa mabavu ambapo kundi la wanajeshi wa Israel walikuwemo humo.
Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon pia umelisambaratisha kwa kombora gari la deraya la wanajeshi wa Israel baina ya kitongoji cha al Mutla na kijiji cha Kfarkela karibu na mpaka wa Lebanon na ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Utawala wa Kizayuni Jumatatu Septemba 23 mwaka huu ulianzisha mashambulizi makubwa dhidi ya maeneo mbalimbali kusini mwa Lebanon; hujuma ambazo zinaendelea hadi sasa.
Hizbullah ya Lebanon haijakaa kimya mbele ya mashambulizi ya jinai za kikatili za Israel dhidi ya raia wa nchi hiyo, ambapo imeanzisha operesheni nyingi za kulipiza kisasi dhidi ya maeneo na vitongoji vya walowezi wa Kizayuni kaskazini mwa Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa kuvurumisha mamia ya makombora.