
Kwa mara nyingine tena wananchi wa Tunisiia wameandamana karibu na ubalozi wa Marekani mjini Tunis na kushinikiza balozi huyo wa dola la kibeberu atimuliwe nchini mwao.
Kwa mujibu wa shirika la habari la FARS, maandamano hayo yamefanyika wakati huu ambapo Marekani inashirikiana kikamilifu na utawala wa Kizayuni wa Israel kufanya jinai katika Ukanda wa Ghaza na Lebanon na kuua na kujeruhia maelfu ya watu wasio na hatia.
Wanaharakati nchini Tunisia wamefanya maandamano hayo usiku wakipaza sauti za kutaka kutimuliwa balozi wa Marekani nchini mwao wakisema: “Balozi za Marekani ni balozi wa kigaidi.”
Hii si mara ya kwanza kwa wananchi wa Tunisia kufanya maandamano ya kushinikiza kutimuliwa balozi wa Marekani nchini mwao.
Mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu, Mamia ya raia wa Tunisia waliandamana na kukusanyika mbele ya ubalozi wa Marekani nchini humo wakilaani jinsi Washington inavyoendelea kushiriki katika mauaji ya umati ya raia wa Ukanda wa Ghaza.
Waandamanaji hao walibeba mabango na maberamu na kutoa mwito wa kutimuliwa balozi wa Marekani nchini Tunisia.
Kwenye maandamano hayo, wananchi wa Tunisia walisikika wakitangaza kwa kubwa kwamba wanalaani siasa za kibeberu za Marekani. Walipaza sauti zao kuliunga mkono taifa madhlumu la Palestina kama ambavyo walisikika pia wakitangaza kwamba rais wa Marekani, Joe Biden ni mtenda jinai.
Ikumbwe kuwa, wananchi wa Tunisia wamekuwa wakimiminika mabarabarani mara kwa mara kufanya maaandamano ya kulaani jinai zinazoendelea kkufanywa na Marekani kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Ghaza na Lebanon.