Kwa mara nyingine, HAMAS yaishukuru Iran kwa msaada wake mkubwa kwa Wapalestina

Msemaji wa Brigedi za Izzuddin Qassam, Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa taarifa muhimu na sambamba na kuishukuru Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa msaada wake mkubwa kwa Muqawama na wananchi wa Palestina amesisitiza kuwa, Operesheni ya Kimbunga cha al Aqsa imetoa mfano wa kipekee wa Muqawama na imeweka historia isiyoweza kufutika.