Kwa kuhofia ‘Nakba II’, nchi 5 za Kiarabu zaiandikia barua US kupinga mpango wa Trump kuhusu Ghaza

Mawaziri wa mambo ya nje wa nchi tano za Kiarabu na Afisa Mkuu wa Palestina wametangaza kuwa wanapinga pendekezo tata la Rais wa Marekani Donald Trump la kuwahamisha kwa nguvu Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza na kuwatafutia makazi mengine katika mataifa jirani.