Kuwakabili Ureno na Ronaldo ‘baraka’

Kocha wa timu ya taifa ya Uhispania, De la Fuente, ametamba kuelekea katika mchezo wao wa fanaili dhidi ya timu ya taifa ya Ureno katika Kombe la mataifa Ulaya (UEFA NATIONS LEAGUE) unaotarajiwa kuchezwa mjini Munich, Ujerumani.

Kocha huyo amesema licha ya timu yake kupigiwa upatu wa kulibeba kombe hilo anaona kwamba mchezo huo utakuwa mgumu hasa kutokana na ubora wa Ureno na nahodha wao, Cristiano Ronaldo.

Mechi hiyo pia inatajwa kama pambano la vizazi kati ya Ronaldo mwenye miaka 40 na kinda wa Uhispania, Lamine Yamal wa miaka 17.

Mechi hiyo itachezwa majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Ujerumani na Ufaransa zitacheza mechi ya mshindi wa tatu pia katika mji wa Stuttgart.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *