Kushiriki Iran katika “Mkutano wa Nchi za Bahari ya Hindi” kuna umuhimu gani?

Duru ya Nane ya Mkutano wa Nchi za Bahari ya Hindi chini ya kauli mbiu “Kuelekea Upeo Mpya wa Ushirikiano wa Baharini” imefanyika tarehe 16 na 17 mwezi huu wa Februari huko Oman kwa kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi ya juu wa nchi 20 wanachama. Oman, India na Singapore kwa pamoja zilikuwa wenyeji wa kongamano hilo.