Kura ya maoni kufanyika mwezi Septemba nchini Guinea

Utawala wa kijeshi nchini Guinea, umetangaza kufanyika kwa kura ya maoni tarehe 21 mwezi Septemba, itakayorejesha taifa hilo kwenye utawala wa kiraia, baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliofanyika miaka tatu uliopita.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Kura hiyo ya maoni itatoa nafasi ya kuandikwa kwa katiba mpya, taifa la Guinea likiwa moja kati ya nchi za Afrika Magharibi ambazo watawala wa kijeshi wamecehewesha kurejeshwa kwa utawala wa kiraia baada ya mapinduzi.

Awali kiongozi wa kijeshi Mamadi Doumbouya alikuwa ametangaza kura hiyo ya maoni kufanyika Disemba 31 mwaka uliopita lakini haikufanyika hatua iliochangia raia kuandamana kushinikiza kufanyika kwa kura hiyo ya maoni.

Wanaharakati na viongozi wa upinzani nchini Guinea wameendelea kukosoa kiongozi wa Kijeshi Mamadi Doumbouya, kwa kuwakamata wakosowaji wake, wakiwemo wanahabari kwa madai ya longo, masharika ya kiraia yakidai ni njama ya Doumbouya kuwanyamazisha wakosawaji ili asalie madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *