
Uchunguzi wa maoni iunaonyesha kwamba kiongozi mkuu wa upinzani nchini Ghana, John Dramani Mahama, atashinda uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao wa Desemba, na kumweka mbele ya mpinzani wake mkuu, mgombea wa chama tawala, Mahamudu Bawumia.
Mahama mwenye umri wa miaka 65 ambaye aliwahi kuwa Rais wa Ghana, na Makamu wa Rais wa sasa wa nchi hiyo Bumia (miaka 60) ndio wagombea wakuu katika uchaguzi wa Desemba 7 wakiwania kuchukua nafasi ya Rais Nana Akufo-Addo, ambaye atang’atuka madarakani Januari mwakkani baada ya kutumikia mihula miwili ya rais wa nchi hiyo mzalishaji mkubwa wa dhahabu kakao.
Kundi la watafiti la Global Infometrics lenye makao yake makuu mjini Accra, lilitoa matokeo ya kura ya maoni Jumatatu wiki hii iliyoonyesha kwamba, Mahama atashinda uchaguzi wa rais kwa asilimia 52, akifuatiwa na Bumia aliyopata asilimia 41.3 katika uchaguzi huo unaowachuanisha wagombea 31.
Utafiti huo ulibaini kuwa wapiga kura wanavutiwa zaidi na uchumi, ajira, elimu na miundombinu, ambayo Mahama aliwekeza kwa kiasi kikubwa katika kipindi chake cha kwanza cha urais kati ya 2012 na 2017, alipokabiliwa na ukosoaji juu ya uhaba wa nishati na kuyumba kwa uchumi.
Serikali ya John Dramani Mahama pia ilihusishwa na tuhuma za ufisadi, ingawa hakuwahi kutuhumiwa moja kwa moja kama rais. Anagombea tena kwa tiketi ya chama cha National Democratic Congress, chama kikuu cha upinzani.