Kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner londoka Mali, na nafasi yake kuchukuliwa na Africa Corps

Kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner linaondoka Mali, ambapo limekuwepo tangu mwaka 2021, na askari wake watajumuishwa tena katika mrithi wake, Africa Corps, shirika lingine lililo chini ya udhibiti wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi, vyanzo vya kidiplomasia na usalama vimeliambia shirika la habari la  AFP siku ya Jumapili.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Tangu mapinduzi mawili ya mwaka 2020 na 2021 ambayo yaliweka wanajeshi mamlakani, utawala wa kijeshi unaoongozwa na Jenerali Assimi Goïta. Mali imevunja mahusiano yake na mkoloni wa zamani wa Ufaransa baada ya kuanzisha mahusiano na Urusi katika nyanja za kijeshi na kisiasa, haswa kwa kutoa wito kwa huduma za Wagner.

“Hatimaye Wagner inasitisha uwepo wake nchini Mali. Lakini Africa Corps inachukua nafasi ya kundi hili la wanamgambo wa Urusi,” chanzo cha kidiplomasia katika Sahel kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumapili.

Ujumbe uliotumwa Ijumaa kwenye kituo cha Telegram unaohusishwa na kundi hilo umepongeza: “Kazi imekamilika. PMC Wagner wanarudi nyumbani.”

Kremlin “Mwalimu wa Mchezo”

“Kremlin inasalia kuwa bingwa wa mchezo,” chanzo hicho cha kidiplomasia kimeongeza: “Wafanyakazi wengi wa Wagner nchini Mali kutoka Urusi wataunganishwa tena katika Africa Corps na kuwekwa katika miji mikuu ya kikanda ya Kaskazini na huko Bamako.”

Kwa muda wa miaka mitatu na nusu, Mali imetoa wito kwa kundi la Wagner kulisaidia katika mapambano yake dhidi ya makundi ya kijihadi ambayo yameua maelfu ya watu katika ardhi yake.

Mali haijawahi kukiri rasmi kuwepo kwa mamluki wa Wagner, lakini inadai kutumia wakufunzi wa Kirusi.

Wagner hutoa huduma mbalimbali kwa serikali zenye matatizo.

Wagner, kundi maarufu zaidi la mamluki la Urusi, lilivunjwa na kupangwa upya kufuatia kifo cha kiongozi wake, Yevgeny Prigozhin, mnamo mwezi 2023, aliyefariki katika ajali ya ndege muda mfupi baada ya jaribio lake la uasi wa kutumia silaha dhidi ya Moscow. Operesheni nyingi za usalama barani Afrika sasa zinaratibiwa na Africa Corps, chini ya udhibiti wa Wizara ya Ulinzi ya Urusi.

“Hakuna mabadiliko”

“Wagner jana au Africa Corps leo, mshirika wetu anabaki kuwa ule ule: nguvu kuu nchini Urusi, ambayo ni, Kremlin,” chanzo cha usalama cha Mali kimesema siku ya Jumapili.

Chanzo cha kijeshi cha Mali kinathibitisha kwamba “Wagner au la, (…) Urusi inasalia kuwa mshirika wetu wa kimkakati katika ushirikiano wa kijeshi.”

Kwa hakika, “hakutakuwa na mabadiliko kwa kuondoka kwa PMC” (Wagner), kinahakikishia kituo cha Telegram chenye mahusiano na na Africa Corps.

Mbinu za kikatili za kundi hilo la wanamgambo nchini Mali zimekuwa zikilaumiwa mara kwa mara na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kutetea haki za binadamu.

Umoja wa Mataifa umelishutumu jeshi la Mali na wapiganaji wa “kigeni” katika ripoti ya kuwaua watu wasiopungua 500 wakati wa operesheni dhidi ya wanajihadi huko Moura, katikati mwa nchi hiyo, mwezi Machi 2022, mashtaka ambayo yalikanushwa na serikali ya Mali.

Kulingana na vyanzo vya Magharibi, wapiganaji hawa wa kigeni ni wanachama wa Wagner.

Mwezi Aprili mwaka jana, miili kadhaa iligunduliwa karibu na kambi ya kijeshi ya Mali, siku chache baada ya jeshi la Wagner na wanamgambo kuwakamata makumi ya raia, wengi wao kutoka jamii ya Fulani.

“Kuongezeka” kwa mashambulizi

Tangazo hili la kuondoka kwa Wagner linakuja huku kukiwa na “kuzuka upya” kwa mashambulizi ya wanajihadi, kulingana na makao makuu ya jeshi la Mali.

Jeshi lililazimika kuondoka katika moja ya kambi zake kuu za kijeshi katikati mwa nchi baada ya mashambulizi mawili yaliyohusishwa na wanajihadi na kuua makumi ya wanajeshi katika muda wa siku chache.

Chanzo cha kidiplomasia cha Ulaya katika Sahel kinabaini kwamba Africa Corps “huenda itafanya mafunzo zaidi kwa jeshi la Mali. Kwa vyovyote vile, mafunzo mengi zaidi kwa wanajeshi wa Mali kuliko Wagner ilivyokuwa ikifanya.”

“Ingawa Wagner inadai kwamba operesheni na uungwaji mkono wake umeimarisha jeshi la Mali, Africa Corps itahitaji kuendelea kutoa mafunzo na usaidizi, haswa baada ya wimbi la hivi majuzi la mashambulizi dhidi ya FAMA (Vikosi vya Wanajeshi wa Mali),” anasema Beverly Ochieng wa Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS).

Mnamo Agosti 2024, jeshi la Mali na Wagner walipata hasara kubwa baada ya kushindwa kwa kiasi kikubwa katika mji wa kaskazini wa Tinzaouatène, kwenye mpaka wa Algeria. Waasi wanaotaka kujitenga na wanajihadi walidai kuwaua makumi ya wanamgambo wa Urusi na wanajeshi wa Mali wakati wa mapigano hayo.

Jeshi na Wagner walikubali hasara kubwa, bila kutoa idadi maalum ya vifo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *