Kundi la Mgogoro: Uasi huko Goma, DRC, Unaweza Kusababisha Vita vya Kikanda

Kundi la International Crisis Group limesema kuwa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuvamia mji wa Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuudhibiti mji huo wenye watu milioni moja.