Kremlin yathibitisha kwa mara nyingine tena nia yake ya kuimarisha ushirikiano wake na Afrika

Kundi la Wagner lilitangaza siku chache zilizopita kwamba linaondoka Mali, ambako lilikuwapo tangu mwaka 2021. Shirika lingine la Kirusi, wakati huu chini ya udhibiti wa moja kwa moja wa Wizara ya Ulinzi, Africa Corps litachukuwa nafasiya Wagner. Kremlin imebainisha sera yake mnamo Jumatatu, Juni 9: kuimarisha uhusiano na bara la Afrika.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutoka kwa mwandishi wetu huko Moscow,

Nia ya kudumisha uhusiano. Bila kutoa maoni moja kwa moja juu ya ushirikiano huu au kurejelea kundi la wanamgambo wa marehemu Yevgeny Prigozhin, huu ndio muktadha wa ujumbe wa Kremlin uliotumwa Jumatatu hii na msemaji wake Dmitry Peskov.

“Uwepo wa Urusi barani Afrika unazidi kuimarika. Tunakusudia kupanua kwa kiasi kikubwa uhusiao wetu na nchi za Afrika. Tunazingatia ushirikiano wa kiuchumi na uwekezaji. Ushirikiano huu unaenea katika nyanja nyeti zinaazohusiana na ulinzi na usalama.” Katika suala hili, Urusi itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake na mataifa ya Afrika,” amesema Dmitry Peskov.

Mnamo Juni 3, kituo cha Telegram cha Afrika Corps kilitangaza kwamba kitaendelea kuajiri wanamgambo wnchini Urusi na kuorodhesha vituo vyake vya uteuzi huko Moscow, St. Petersburg, Kazan, na Novorossiysk, kusini mwa nchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *