
KITENDO cha Coastal Union kutupwa nje ya mashindano ya Kombe la Muungano baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Zimamoto katika hatua ya robo fainali, kaimu kocha mkuu wa kikosi hicho, Joseph Lazaro amesema nguvu zao wanazielekeza Ligi Kuu Bara.
Coastal Union ilikuwa timu ya pili kutoka Bara kuondoshwa katika mashindano hayo, baada ya awali Singida Black Stars iliyofungua pazia kutupwa nje kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penalti 6-5 na JKU, kufuatia sare ya mabao 2-2.
Akizungumza na Mwanaspoti, Lazaro alisema sababu ya kuondoshwa mapema katika michuano hiyo ni kutokana na kutowajua vyema wapinzani wao, ingawa kwa sasa wanarudi kujipanga upya kwa michezo ijayo ya kumalizia msimu huu wa Ligi Kuu Bara.
“Hayakuwa malengo yetu kutolewa mapema namna hii, ingawa nawashauri waandaaji wabadilishe huu mfumo ili watoe nafasi ya timu zote kucheza zaidi ya mechi moja hadi kufikia mtoano, tumepoteza ila tunajipanga tena na Ligi Kuu,” alisema Lazaro.
Kocha huyo anayekaimu nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Juma Mwambusi, alisema hawatokuwa na mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo, kwani wanahit