Korea Kusini: Washington yampongeza Rais Mteule na inataja muungano “usiovunjika”.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio amempongeza Rais mpya wa Korea Kusini Lee Jae-myung siku ya Jumanne Juni 3 na kueleza nia yake ya kufanya kazi na kiongozi huyo wa mrengo wa kati.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo mbili zimeunganishwa na “muungano usioweza kuvunjika na Mkataba wetu wa Ulinzi wa Pamoja, maadili yetu ya pamoja, na uhusiano wetu wa kina wa kiuchumi,” Rubio amesema katika taarifa, na Marekani ikisalia kuwa mdhamini wa jadi wa usalama wa Korea Kusini.

Mgombea wa kiliberali nchini Korea Kusini,  Lee Jae-myung, ameshinda uchaguzi wa urais nchini humo dhidi ya mpinzani wake wa kihafidhina Kim Moon Soo na ambaye shirika la habari la nchini humo, Yonhap limeripoti kwamba amekubali kushindwa katika uchaguzi huo.

Kulingana na Yonhap, Lee ameshinda kwa asilimia 49.4 ya kura, wakati Kim akipata asilimia 41.1 huku idadi ya wapiga kura ikitajwa kuwa ilikuwa karibu asilimia 80.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *