
Nchini Korea Kusini, “sakata” dhidi ya rais inaendelea. Moon Jae-in hapo awali alikuwa rais pekee wa zamani aliyeepushwa na matatizo na mahakama, lakini ameshtakiwa kwa ufisadi silku ya Alhamisi, Aprili 24. Rais huyo wa zamani wa mrengo wa kati anashutumiwa kwa kuwezesha kuajiriwa kwa mkwewe. Kipindi kingine katika machafuko ya kisiasa ya Korea Kusini tangu Rais Yoon aliposhindwa kutangaza sheria ya kijeshi.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Alikuwa kiongozi mwadilifu, anayejulikana kwa sera yake ya wazi dhidi ya Korea Kaskazini, rais pekee wa zamani wa Korea Kusini ambaye bado yuko hai ambaye ameepusha matatizo na mahakama nchini mwake. Moon Jae-in pia hatimaye atakabiliwa na mashtaka ya ufisadi.
Rushwa
Upande wa mashtaka unabaini kwamba mkwe wa rais wa mrengo wa kati alipata kazi kinyume cha sheria. Aliteuliwa kuwa meneja mkuu wa Thai Easter Jet, kampuni inayoendeshwa na mbunge wa zamani kutoka chama cha democratic cha Moon Jae-in. Waendesha mashtaka wanadai kuwa mshahara wa euro 132,000 uliopokelewa ulikuwa hongo kwa rais. Kwa sababu hii iliruhusu binti yake na mkwe wake kuishi bila msaada wa kifedha wa wazazi wao.
Kizimbani kwa miaka kadhaa
Shutuma za ufisadi zinachukuliwa kwa uzito nchini Korea Kusini, na wakuu kadhaa wa nchi wamelengwa. Kama Lee Myung-bak na Park Geun-hye, marais wawili wahafidhina ambao walitumia miaka kadhaa gerezani kwa sababu hii. Yoon Suk-yeol, anayetuhumiwa kwa uasi kwa kutangaza sheria ya kijeshi, kwa sasa yuko mahakamani na anakabiliwa na kifungo cha maisha.