Korea Kusini : Mahakama ya katiba yaunga mkono kutimuliwa kwa rais Yoon Suk Yeol

Majaji wa Mahakama ya Katiba nchini Korea Kusini, kwa kauli moja, wameamua kuunga mkono kuondolewa madarakani kwa rais Yoon Suk Yeol na bunge mwezi Desemba mwaka uliopita.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Baada ya uamuzi huo wa Mahakama, kumekuwa na furaha kubwa kutoka kwa wapinzani wa Yoon jijini Seoul, huku wafuasi wake wakionekana wenye huzuni.

Majaji katika uamuzi wake wamebaini kuwa Yoon, alikiuka katiba baada ya kuagiza matumizi ya sheria za kijeshi na hatua ya wabunge kumwondoa madarakani, ilikuwa sahihi.

Polisi wameonekana kuwa katika hali ya tahadhari, kuepusha uwezekano wa kutokea kwa makabiliano kati ya makundi hayo mawili.

Majaji katika uamuzi wake wamebaini kuwa Yoon, alikiuka katiba baada ya kuagiza matumizi ya sheria za kijeshi na hatua ya wabunge kumwondoa madarakani, ilikuwa sahihi.
Majaji katika uamuzi wake wamebaini kuwa Yoon, alikiuka katiba baada ya kuagiza matumizi ya sheria za kijeshi na hatua ya wabunge kumwondoa madarakani, ilikuwa sahihi. © Song Kyung-Seok / Reuters

Baada ya uamuzi wa Mahakama, kwa mujibu wa katiba, uchaguzi mpya unapaswa kufanyika baada ya siku sitini, kumchagua rais mpya.

Chama cha rais huyo aliyeondolewa madarakani, People Power, kimesema kimekubali uamuzi wa Mahakama ya Katiba na kuomba radhi kwa wananchi wa Korea Kusini.

Kiongozi mkuu wa upinzani Lee Jae-myung, naye amepongeza hatua ya Mahakama na kumshtumu kiongozi huyo wa zamani kwa kutishia demokrasia ya nchi hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *