
Watu 19 wamefariki katika mfululizo wa moto wa misitu miongoni mwa matukio mabaya zaidi katika historia ya Korea Kusini, ambao umesababisha uharibifu usio na kifani.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Helikopta iliyotumwa kukabiliana na moto unaoteketeza kusini mashariki mwa nchi “imeanguka siku Jumatano Machi 26 katika eneo la milima la Uiseong County,” na kumuua rubani wake, idara ya zimamoto ya mkoa wa Gyeongbuk (mashariki) imeliambia shirika la habari la AFP.
Watu wengine 18 wamefariki katika moto huo, afisa wa wizara ya usalama ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatano, akiongeza kuwa watu sita wamejeruhiwa vibaya na kumi na watatu kujeruhiwa kidogo.
Moto huo umefika haraka sana hadi watu wamekimbia bila kuchukua mali yoyote, wakaazi ambao walikuwa wamekimbilia katika uwanja wa mazoezi wa Shule ya Msingi ya Sinsung wameliambia shirika la habari la AFP.
“Upepo ulikuwa mkali sana,” amesema Kwon So-han, mkazi wa Andong mwenye umri wa miaka 79 ambaye amekimbia mara tu alipopokea agizo la kuhama.
“Moto ulitoka mlimani na kugonga nyumba yangu,” amesema, akidai kuwa hakuweza kuchukua chochote.
“Uharibifu ambao haujawahi kutokea”
Moto huu “umesababisha uharibifu ambao haujawahi kutokea,” kaimu Rais Han Duck-soo amesema, akibainisha kwamba “wanaendeleza kwa njia inayozidi mifano ya utabiri iliyopo.”
Bw. Han amesema kiwango cha tahadhari hadi kiwango cha juu zaidi Jumatano na akatangaza “mwitikio kamili wa kitaifa.”
Mamia ya wanajeshi wamehamasishwa kukabiliana na mioto mingi, na jeshi la Marekani linatoa msaada wa helikopta kutoka kambi zake za kijeshi kusini mwa nchi hiyo, kulingana na rais wa mpito.