
Korea Kaskazini imerusha “makombora kadhaa ya balestiki yasiyotambulika” Jumatatu, Machi 10, jeshi la Korea Kusini limetangaza, siku ambayo Korea Kusini na Marekani zimeanza luteka yao kubwa ya kijeshi ya kila mwaka, Freedom Shield, linaandika shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
“Jeshi letu limegundua karibu saa 7:50 mchana (sawa na 11:50 Alfajiri saa za Ufaransa) makombora kadhaa ya balestiki yasiyotambulika yaliyorushwa kutoka Mkoa wa Hwanghae kuelekea Bahari ya Magharibi,” makao makuu ya majeshi imesema, ikitumia jina la Kikorea la Bahari ya Njano.
Hapo awali, wizara ya mambo ya nje ya Pyongyang, iliyonukuliwa na vyombo vya habari vya serikali, ililaani mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini kuwa ni “uchokozi hatari ambao unazidisha mvutano” na kuonya juu ya hatari ya kuzuka kwa vita kwa “urushaji wa kombora kwa bahati mbaya,” siku chache baada ya jeshi la anga la Seoul kushambulia kimakosa kijiji kimoja katika ardhi yake.
Zoezi la pamoja kati ya Washington na Seoul litajumuisha “mafunzo ya moja kwa moja, ya mtandaoni na ya uwanjani,” kulingana na taarifa ya Marekani. Zoezi hilo linaendelea hadi Machi 21, kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari.
Ushirikiano wa kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini mara kwa mara umeshtumiwa na Pyongyang, ambayo serikali yake inaona mazoezi hayo kama maandalizi ya uvamizi na mara nyingi hufanya majaribio ya makombora kujibiwa.
Mazoezi ya hivi punde yanakuja baada ya ndege mbili za jeshi la anga la Korea Kusini kudondosha mabomu manane kwa bahati mbaya kwenye kijiji kimoja wakati wa mazoezi ya pamoja na wanajeshi wa Marekani mnamo Machi 6. Watu 15, wakiwemo raia na wanajeshi, walijeruhiwa katika tukio hilo, Shirika la taifa la Zimamoto la Korea Kusini limesema.
Uhusiano kati ya Pyongyang na Seoul unazidi kudoroa kwa miaka, kadhaa huku Korea Kaskazini ikirusha mfululizo wa makombora ya balestiki mwaka jana kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa. Korea mbili zimesalia katika vita vya kiufundi, kwani mzozo wa miaka ya 1950-53 ulimalizika kwa vita, sio mkataba wa amani.