
Korea Kaskazini inaandaa mashindano yake ya kwanza ya riadha za Kimataifa katika muda wa miaka sita huko Pyongyang leo Jumapili, ikiwakaribisha wanariadha wa kigeni katika nchi iliyojitenga ambayo kwa kiasi kikubwa imefunga mipaka yake wakati wa janga la UVIKO-19.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Wanariadha kutoka China, Romania na nchi zingine wamewasili Korea Kaskazini kushiriki katika hafla hiyo, shirika la habari la seikali ya China, KCNA, na Rodong Sinmun yameripoti siku ya Jumapili.
Takriban wasafiri 200 wako Pyongyang tangu siku ya Ijumaa na Jumamosi, na wakimbiaji wa kigeni wamepata mafunzo katika hoteli ya Pyongyang kwa ajili ya mashindano ya Jumapili, amesema Simon Cockerell, meneja mkuu wa Koryo Tours yenye makao yake Beijing, katika machapisho ya Instagram yanayoonyesha mitaa ya Pyongyang na eneo la burudani.
Koryo Tours ni mshirika rasmi wa Pyongyang Marathon na husaidia kupanga usajili kwa wageni wa kimataifa.
Korea Kaskazini iliyojitenga ilifunga mipaka yake mnamo mwaka 2020 mwanzoni mwa janga la UVIKO-19, lakini imekuwa ikiondoa vizuizi hatua kwa hatua tangu mwaka 2023. Imeruhusu makundi mengine ya watalii wa Urusi kuingia nchini, lakini mji mkuu wake unaendelea kufungwa kwa utalii wa kawaida.
Mashindano ya Riadha ni mwendo wa kwenda na kurudi kupitia katikati mwa Pyongyang, kupitia eneo lakimkakati la Pyongyang, kuelekea mashambani nje ya katikati mwa jiji na kurudi kwenye uwanja wenye umati wa watu 50,000, kulingana na Koryo Tours.
Mashindao ya Kimataifa za Pyongyang ni mojawapo ya matukio ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Kim Il Sung, mwasisi wa Korea Kaskazini na babu wa kiongozi wa sasa Kim Jong Un.