Korea Kaskazini ilituma wanajeshi 3,000 wa ziada nchini Urusi mwaka huu, Seoul inasema

Korea Kaskazini ilituma wanajeshi 3,000 wa ziada nchini Urusi mwaka huu, pamoja na maelfu ambayo tayari yametumwa kusaidia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, jeshi la Korea Kusini limesema leo Alhamisi, na kuongeza kuwa Pyongyang pia imeendelea kuipatia Moscow makombora, mizinga na zana.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

“Inakadiriwa kuwa wanajeshi 3,000 zaidi walitumwa kama nyongeza kati ya mwezi wa Januari na Februari,” makao makuu ya jeshi laKorea Kusini imetangaza, na kuongeza kuwa wanajeshi 4,000 wa Korea Kaskazini waliuawa au kujeruhiwa kati ya 11,000 waliotumwa hapo awali nchini Urusi.

Urusi na Korea Kaskazini, washirika wa jadi, wameimarisha uhusiano tangu Moscow ilipovamia Ukraine mwaka 2022. Moscow wala Pyongyang hajathibitisha au kukanusha kuwepo kwa wanajeshi wa Korea Kaskazini nchini Urusi hadi sasa. Hata hivyo, nchi hizo mbili zilihitimisha mkataba wa usalama na ulinzi mnamo mwezi wa Juni 2024, wakati wa ziara ya Rais wa Urusi Vladimir Putin nchini Korea Kaskazini.

“Kiasi kikubwa” cha silaha zinazotolewa “

Mbali na wanajeshi, Korea Kaskazini inaendelea kusambaza makombora, vifaa vya mizinga na risasi,” inasema makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini. “Hadi sasa, Korea Kaskazini inakadiriwa kuwa imetoa kiasi kikubwa cha makombora ya masafa mafupi ya balestiki (SRBM), pamoja na takriban vitengo 220 vya bunduki zinazojiendesha zenye milimita 170 vifaa vingine vya kijeshi,” chanzo hicho kimesema. JCS ilionya kwamba “idadi hizi zinaweza kuongezeka kulingana na hali kwenye uwanja wa vita.”

Uhusiano kati ya Pyongyang na Seoul umedororora kabisa kwa miaka kadhaa, na Korea Kaskazini ilirusha mfululizo wa makombora ya balestiki mwaka jana kinyume na vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Wataalamu wamekadiria kuwa jeshi la Korea Kaskazini lenye silaha za nyuklia linaweza kufanya majaribio ya silaha zinazokusudiwa kusafirishwa kwenda Urusi kwa matumizi dhidi ya Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *