KONGAMANO LA KISAYANSI LAFANYIKA DODOMA,LAWAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA AFYA

 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe, akizungumza leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma wakati akifungua kongamano la Kisayansi   katika kuelekea Maadhimisho ya   wiki ya Afya Kitaifa 2025 kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama.

Mganga Mkuu wa Serikali,Dk Grace Maghembe,akizungumza wakati  wa  kongamano la Kisayansi   katika kuelekea Maadhimisho ya   wiki ya Afya Kitaifa 2025 jijini Dodoma .

Sehemu ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,(hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la Kisayansi  katika kuelekea Maadhimisho ya  wiki ya Afya Kitaifa 2025 kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma.

Sehemu ya Washiriki wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,(hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la Kisayansi  katika kuelekea Maadhimisho ya  wiki ya Afya Kitaifa 2025 kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  kongamano la Kisayansi   katika kuelekea Maadhimisho ya   wiki ya Afya Kitaifa 2025 kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  kongamano la Kisayansi   katika kuelekea Maadhimisho ya Wiki ya Afya Kitaifa 2025 kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imesema  itaendelea kuimarisha Mfumo wa Utafiti na kutumia matokeo,kutenga fedha za kufanyia tafiti na  kusimamia tafiti lengo likiwa ni kuzidi kuiboresha sekta ya afya.
Hayo yameelezwa leo Aprili 4,2025 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe,  kwa niaba ya Waziri wa Afya,Jenista Mhagama wakati akifungua kongamano la Kisayansi  katika kuelekea Maadhimisho ya  wiki ya Afya Kitaifa 2025.
Dk Shekalaghe amesema Utafiti wa magonjwa ya binadamu ni muhimu katika kuboresha huduma za afya na Kinga ambapo amedai Serikali itahakikisha inazitumia tafiti hizo.
“Miradi mingi ya Utafiti imetekelezwa na  Serikali imefanya mambo makubwa kwa kusaidiwa na tafiti hizo  ambapo dhamira ni kuimarisha tafiti kwa kutumia tafiti.”amesema Dkt.Shekalaghe
Kwa upande wake,Mganga Mkuu wa Serikali,Dk Grace Maghembe amesema wameona hawawezi kuadhimisha wiki ya Afya bila kuwa na majadiliano ya kitaaluma.
Amesema forum hiyo imeleta wataalamu mbalimbali lengo ni kupata mawasilisho mbalimbali katika sekta ya afya,kubadiishana uzoefu na kuona namna gani ya kufanya vizuri zaidi.
Pia watapata Nafasi ya kujifunza kupitia wale ambao wanaofanya vizuri zaidi 
Amesema kupitia kauli mbiu tulipotoka tuendapo na tulipo katika sekta ya afya watajifunza mambo mbalimbali huku kwa upande wa tafiti wameweka wabobevu na wale wanaoelekea katika ubobovu.
Naye Mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  (TAMISEMI),Dk Rashid Mfaume amesema wanajivunia maboresho katika sekta ya afya kwa  kuwezesha vituo vya Afya kundaa mipango yao wenyewe.
Dk Mfaume ambaye ni Mkurugenzi wa Afya na Lishe Tamisemi amesema wanajivunia mifumo imara katika sekta ya afya ambayo imesaidia upatikaji wa bidhaa za afya kwa kuzidi kuimarika.
“TAMISEMI imeanza kusimamia suala la bima ya Afya kwa wote.Tunamshukuru Sana Mheshimiwa Rais kwenye rasilimali watu kwani katika kipindi Cha miaka minne zaidi ya watumishi 25,000 wameajiriwa.Hospitali 129 mpya zimejengwa majengo zaidi ya 14,”amesema Dk Mfaume.
Kwa upande wake,Mkuu shule ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)  Prof Steven  Kigusi amesema  wao ni sehemu muhimu kama wadau katika sekta ya afya na dhamira yao ni kuendeleza wataalamu wa Afya wenye ujuzi kupitia shule zao udaktari na Uuguzi.
Amesema wanaendelea kuboresha huduma za afya kwa kuona huduma bora za afya zinawafikia watanzania wengi.
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dk Edwin Swai amesema wataendelea kufanya tafiti lengo likiwa ni kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zote zinazoikabili sekta ya afya.

The post KONGAMANO LA KISAYANSI LAFANYIKA DODOMA,LAWAKUTANISHA WADAU WA SEKTA YA AFYA appeared first on Mzalendo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *