Kongamano la Chakula Ulimwenguni lafunguliwa kwa wito wa kuunda mifumo jumuishi ya chakula

Kongamano la Chakula Ulimwenguni lilianza Jumatatu huko Roma chini ya mada, ‘Chakula kizuri kwa wote, leo na kesho.’

Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) Qu Dongyu ametoa wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya chakula na kilimo kama njia ya kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Ameongeza kuwa: “Hatua tunazochukua leo zitaathiri moja kwa moja siku zijazo,  Kauli hiyo  mbiu ya mwaka huu, ‘Chakula Bora kwa Wote, Leo na Kesho,’ inaakisi kiini cha dhamira ya FAO na kuleta pamoja umuhimu wa Mambo Nne Bora, uzalishaji bora, lishe bora, mazingira bora na maisha bora, bila kuacha mtu nyuma.”

Viongozi wa Liberia, Lesotho na Eswatini pia wako kwenye kongamano hilo wamebainisha katika hotuba zao kuwa nchi za Kiafrika zilikuwa zikipambana katika lengo lao la kufikia sifuri la njaa, lililochanganyikiwa na migogoro, magonjwa ya milipuko na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mfalme Mswati III wa Eswatini amehutubu katika kikao hicho na kusema: “Tunapoangalia kuendeleza bidhaa zetu za chakula, hili halitawezekana bila miundombinu wezeshi, mfano barabara, maghala na TEHAMA.”

Katika muda wa siku tatu zijazo, wataalam wa kimataifa, vijana wenye kuleta mabadiliko, wawekezaji, na viongozi watajadili hatua zinazohitajika kufikia mifumo endelevu na jumuishi ya kilimo cha kimataifa.

Katika Afrika, zaidi ya watu milioni 340 wameainishwa kama wasio na uhakika wa chakula kulingana na ripoti ya mwaka  2023 ya FAO.