Dar es Salaam. Mambo yanazidi kumnyookea kocha wa timu ya wanawake ya Yanga ‘Yanga Princess’ baada ya kuongezwa kwenye benchi la ufundi la kikosi cha wakubwa wanaume.
Lema maarufu kwa jina la Mourinho sasa ataungana na kocha mkuu Hamdi Miloud na wasaidizi wake wengine katika benchi la timu hiyo.
Yanga imechukua hatua hiyo ikiwa ni mpango wa uongozi wa timu hiyo chini ya Rais injinia Hersi Said na Miloud kuunganisha idara za ufundi za timu hiyo.
Mpango huo unalenga kutaka kuona mifumo ya ufundi inawiana ambapo Lema ambaye ni kocha wa kikosi cha wasichana Cha Yanga Princess anazinasa falsafa za Miloud.

Lema ataanza kuhudhuria mazoezi ya timu hiyo ya wakubwa kuanzia Leo ilijiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union ambapo pia atakuwa kwenye benchi hata kwenye mechiezo hiyo.
Kocha huyo amepata muda huo baada ya kusimama kwa mechi za Ligi ya wanawake ambapo kikosi chake kinashika nafasi ya tatu.
Mwezi uliopita, Edna Lema aliiongoza Yanga Princess kutwaa ubingwa wa mashindano ya Samia Women’s Super Cup baada ya kuifunga JKT Queens kwa mabao 3-0.