
BAADA ya kukusanya pointi 38 na kukaa kileleni, Kocha wa JKT Queens, Esther Chabruma amesema wanaandaa mikakati ya kupata pointi 12 za kuwania ubingwa.
JKT hadi sasa ndiyo pekee ambayo haijapoteza mchezo wowote Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na katika mechi 14 imeshinda 12 na sare 12, ikifunga mabao 56 tofauti ya mabao 10 na Simba yenye 46, ikiwa nafasi ya pili na pointi 38.
Akizungumza na Mwanaspoti, Chabruma alisema kwa upande wao hawana mechi ndogo na mikakati yao ni kuhakikisha timu hiyo inashinda kila mchezo na kujiweka salama kwenye mbio za ubingwa.
Aliongeza, ingawa ni mechi ngumu lakini wakijipanga kila kitu kinawezekana akiwapongeza wachezaji wake ambao licha ya kukumbana na changamoto mbalimbali hawajamuangusha.
“Mechi zote ngumu kwa sababu unapokuwa kwenye mbio za kuwania ubingwa hata timu ndogo zinapokutana na timu kubwa zinapambana kujikwamua, hatuna namna zaidi ya kupambana zaidi,” alisema Chabruma.