Kocha Alliance aeleza kilichowaponza kwa Yanga Princess

KOCHA Mkuu wa Alliance Girls, Sultan Juma amesema kilichowaponza kudondosha pointi dhidi ya Yanga Princess ni pamoja na kuchelewa kwa vibali vya wachezaji wake.

Wikiendi iliyopita timu hiyo ilipoteza mbele ya Yanga Princess ikichapwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sultan alisema takribani wachezaji sita waliopandishwa kwenye kituo cha timu hiyo hawakuwa na vibali vilivyomfanya abadilishe na kuwatumia wachezaji wengine.

“Sasa mambo yako freshi na naweza kuwatumia kwenye mchezo ujao. Vibali vyao vilichelewa kwa sababu unapopandisha wachezaji lazima uwe umewalipa. Kulikuwa na mambo mengi hasa msiba uliwavuruga viongozi,” alisema Sultan.

Wiki hii timu hiyo itakuwa Uwanja wa Nyamagana Mwanza kuikaribisha Fountain Gate Princess na hapa anaeleza maandalizi yao: “Tumejiandaa vizuri huu ni kama mchezo wa dabi kwani timu zote mbili ni za akademi.”