Kissu Naibu Mkurugenzi ya Mawasiliano Ikulu

Dar es Salaam. Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Africa Media Group, Shaaban Kissu, kuwa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Taarifa ya uteuzi wa Kissu, imetolewa leo, Jumatano, Mei 7, 2025 na Katibu wa Rais, Waziri Salum katika hafla ya chakula cha mchana kati ya Rais Samia na wanahabari walishiriki tuzo za Samia Kalamu Awards.

Katika taarifa hiyo, Salum amemtambulisha Kissu katika wadhifa huo mpya, huku akisema uteuzi wake umefanywa leo na hata mwenyewe hakuwa na taarifa.

Kissu amepokea taarifa hiyo, akiwa mshereheshaji katika hafla hiyo.

“Hii taarifa nafikiri ni surprise hata kwa Kissu mwenyewe, kwa sababu hakuwa na taarifa. Hata mmeona nimechelewa kufika hapa tulikuwa tunashughulikia mambo hayo,” amesema Salum akimwakilisha Rais Samia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *