Kipenga cha uchaguzi mkuu 2025 kimepulizwa Tanzania

2025 ni mwaka unaotarajiwa kutawaliwa na matukio mengi ya kisiasa nchini Tanzania kutokana na uwepo wa uchaguzi mkuu wa urais wa Muungano na Zanzibar. Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na Madiwani katika kata zipatazo 4,000 nchi nzima.