
Kiongozi wa upinzani nchini Tanzania Tundu Lissu, ambaye amekuwa akikabiliwa na kesi ya uhaini tangu akamatwe mwezi uliopita, ataanza mgomo wa kula, wakili wake ametangaza siku ya Jumamosi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inajiandaa kwa uchaguzi mwezi Oktoba, lakini Bw. Lissu, kiongozi wa chama cha upinzani cha Chadema, anakabiliwa na hukumu ya kifo iwapo atapatikana na hatia ya uhaini.
“Lissu atagoma kula hadi haki itendeke,” mwanasheria wake, wakili Peter Kibatala amewaambia waandishi wa habari na kuongeza kuwa mgomo huo utaanza Jumapili au Jumatatu.
“Yuko tayari kwa lolote,” Bw. Kibatala amesema.
Lissu, 57, anapinga kuzuiliwa kwa mawakili wake na familia yake kufika gerezani, pamoja na vikwazo vya kuhudhuria kwa watu katika kesi yake anapofikishwa mahakamani, wakili huyome.
Aprili 24, polisi waliwapiga wafuasi wa Chadema walipokuwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa Bw. Lissu tangu kufunguliwa mashtaka.
Alikataa kuhudhuria, kwa vile mamlaka ilisisitiza kuwa anaweza tu kuonekana kwa njia ya video.
Lissu amekamatwa mara kadhaa kwa miaka mingi na kuponea chupuchupu katika jaribio la mauaji mwaka 2017.
Chama chake, Chadema, kilimtuhumu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kurejesha mbinu kandamizi za mtangulizi wake, John Magufuli.
Chadema ilitangaza mapema mwaka huu kuwa itasusia uchaguzi wa mwezi Oktoba ikiwa hakuta kuwa na mageuzi yoyote, ikiwamo tume huru ya uchaguzi na kanuni zilizo wazi zaidi za kuhakikisha wagombea wake hawaondolewi kwenye sanduku la kura.
Chama baadaye kilienguliwa kwenye uchuguzi kwa kukataa kutia saini “kanuni za maadili” za uchaguzi.