Kiongozi wa Syria afanya ziara ya kwanza mjini Daraa

Shirika la habari la serikali, SANA, lilichapisha picha za video zikionyesha umati wa watu wakimshangilia Sharaa, wakati wa ziara hiyo, iliyofanyika katika sikukuu ya Kiislamu ya Eid al-Adha.

Sharaa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani, Anas Khattab, walitembelea msikiti wa kihistoria wa Omari uliopo Daraa. Sharaa alikutana pia na maafisa wa kiraia na kijeshi wa eneo hilo, pamoja na ujumbe kutoka kwa jamii ya Wakristo waliowachache.

Gavana wa mkoa wa Daraa, Anwar al-Zoabi, alisema kuwa ziara hiyo ni “hatua muhimu katika mchakato wa urejeshwaji wa mshikamano wa kitaifa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *