Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu: Mpango wa kijinga wa Marekani kuhusu Gaza hautafika popote

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, akiwapongeza wapiganaji wa Muqawama kwa ushindi wao katika Ukanda wa Gaza, amesisitiza kwamba kazi kubwa ya viongozi na wapiganaji wa Muqawama wa Palestina ipo katika “umoja na mshikamano” na “kusimama imara” dhidi ya adui, kuendesha mchakato mgumu wa mazungumzo, pamoja na uvumilivu na ustahimilivu wa wananchi, ambavyo vimeinua heshima ya Muqawama katika eneo.