Kiongozi wa Mapinduzi: Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ametuma salamu na ujumbe maalumu kwa mnasaba wa kufanyika mazishi na maziko ya Mwanajihadi mkubwa Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Shahidi Sayyid Hashem Safiyyuddin na kusisitiza kuwa: “adui ajue kwamba, Muqawama wa kukabiliana na ughasibu, dhulma na uistikbari si wa kumalizika; na kwa idhini ya Allah utaendelea hadi ufikie lengo ulilokusudia”.