Kiongozi Muadhamu: Iran inakabiliwa na muungano wa madola ya kinafiki

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei amesema Jamhuri ya Kiislamu haina tatizo na mataifa mengine; lakini hata hivyo inakabiliwa na muungano mpana wa “madola ya kinafiki” yanayojaribu kuingilia mambo yake ya ndani na kuvuruga uhusiano wake wa nje.